Tarehe : Aug. 31, 2018, 7:27 a.m.
Na Asteria Muhozya,
Kuanzia tarehe 21, 23 na 24 Agosti, Wizara ya Madini ilikutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambapo taarifa mbalimbali za Utekelezaji wa Majukumu na Miradi zimewasilishwa.
Baadhi ya taarifa zilizowasilishwa katika vikao hivyo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume ya Madini kuanzia mwezi Aprili hadi Julai,2018,
Taarifa kuhusu Uendelezaji na Uwekezaji katika Madini Mkakati na
Taarifa kuhusu Uendelezaji ya Migodi ya Makaa ya Mawe.
Aidha, katika vikao hivyo, Kamati ilitoa maagizo mbalimbali yanayopaswa kufanyiwa kazi na Wizara ili kuboresha Sekta ya Madini nchini.
* ALICHOKISEMA WAZIRI WA MADINI ANGELLAH KAIRUKI
# Graphite ni madini ambayo tunayapa kipaumbele. Ninawaomba wananchi na ninyi Waheshimiwa Wabunge mtusaidie kuwaambia wananchi wasikwamishe miradi ya uwekezaji.
# Tutakapokuwa katika hatua za uchimbaji wa madini ya Urani, tutakuwa karibu sana na kila hatua itakayofanyika kuhakikisha kwamba hakuna athari zozote za kijamii. Serikali haitaweka maslahi ya kiuchumi mbele kuliko ya kijamii.
# Tutafanya Jukwaa kubwa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini mwaka 2019. Lengo ni kuvutia Wawekezaji na kuwakutanisha wachimbaji na Wabia lakini pia Taasisi za Kifedha.
*ALICHOKISEMA NAIBU WAZIRI WA MADINI, DOTO BITEKO
# Wachimbaji wetu wanahitaji huduma za umeme, maji na barabara katika maeneo yao. Yapo baadhi ya maeneo ambayo tayari Mhe. Waziri amewasiliana na Mamlaka husika kwa ajili ya masuala hayo.
* ALICHOKISEMA NAIBU WAZIRI WA MADINI STANSLAUS NYONGO
# Tuna madini mengi ya Kimkakati. Tunaangalia madini ambayo yatasaidia kusukuma mbele Sekta ya Viwanda.
* ALICHOKISEMA KATIBU MKUU WIZARA YA MADINI, PROF. SIMON MSANJILA
# Kama Wizara tunayo nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. Tunaangalia mfumo mzuri wa namna ya kuwasaidia. Tutawashirikisha Waheshimiwa Wabunge kuhusu namna ya kufanya jambo hilo kwa ubora zaidi.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.