[Latest Updates]: Prof. Msanjila awataka STAMICO kuutangaza mtambo wa kuchoronga miamba

Tarehe : Dec. 24, 2018, 10:17 a.m.
left

Na Nuru Mwasampeta

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutumia mtambo wa kuchoronga miamba kwa ufanisi ili kuliletea tija Taifa pamoja na  shirika hilo kutokana na  kipato kitakachotokana na uwepo wa mtambo huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Nsajigwa Kabigi, akieleza jambo kuhusu mtambo huo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (mwenye tai) na wajumbe walioshiriki katika tukio hilo.[/caption]

Ameyasema hayo leo Desemba 24, 2018 wakati wa hafla fupi ya kuukabidhi rasmi mtambo huo kwa STAMICO kwa ajili ya kuanza kuutumia.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Prof. Msanjila amesema, ununuzi wa mtambo huo ni uwekezaji mkubwa ambao Serikali imeufanya kwa shirika la Stamico hivyo, halina kuutumia vyema ili uweze kuleta tija.

Akizungumzia gharama za mtambo huo, Prof. Msanjila amesema umegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja na laki tatu(USD 1.3) ambazo yeye kama Mtendaji Mkuu wa wizara anaona kuwa na deni kubwa kwake, na hivyo kuahidi kuusimamia ipasavyo ili kuhakikisha mtambo huo unazalisha faida na kuwa chachu ya kuweza kununua mitambo mingine  kama hiyo ili kukuza sekta ya madini nchini.

Aidha, amelitaka Shirika hilo kujitangaza vema ili wananchi na hususn wadau wa madini wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini kufahamu uwepo wa mtambo huo ili uweze kutumika hata kwa kampuni binafsi ili kujiongezea kipato lakini pia kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. “Kwa zabuni nilizozisikia mpaka sasa mtambo huu utazalisha pesa za kutosha” amesema Msanjila.

Mbali na kukabidhi mtambo huo, Prof. Msanjila ameitaka Stamico kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi ya mtambo huo kila robo ya mwaka ili kuweza kufanya tathmini endapo mtambo unatumika kwa faida.

Pia, ameliagiza shirika hilo kuhakikisha kuwa, mtambo huo unawezesha manunuzi ya mtambo mwingine mpya kila mwaka ili ndani ya miaka mitano shirika liweze kumiliki mitambo mitano na kurahisisha utekelezaji wa shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini.

Akizungumzia ubora wa mtambo huo, Mkurugenzi wa Kampuni  ya Geo field Tanzania Ltd Denis Dillip ambaye ndiye mnunuzi wa mtambo huo amesema, mtambo huo ni wa kisasa na unatumika katika kuchimba aina tatu za miamba lakini pia unaweza kutumika katika kuchimba visima vya maji.

Aidha, Denis ameishukuru Serikali kwa wazo la kununua mtambo huo na kukiri kuwa, utawasaidia wchimbaji wadogo katika kuendeleza kazi zao za uchimbaji na utafutaji wa madini.

Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali na Utawala, Nsajigwa Kabigi mara baada ya kuwasili katika ofisi za STAMICO kwa ajili ya makabidhiano ya mtambo wa kuchoronga miamba. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku.[/caption]

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kanali Sylvester Ghuliku amekiri kuwa mtambo huo ni talanta waliyopewa na serikali na kuahidi kutoifukia na badala yake watahakikisha unatumika kwa faida na kuhakikisha unazalisha faida kwa serikali.

“Dola za kimarekani milioni 1.3 mlizotuamini na kutukabidhi ni pesa nyingi sana, na hamjatukabidhi ili zikae kwenye makabati, tutahakikisha tunautumia mtambo huu kwa weledi mkubwa ili uweze kuleta tija, ni imani yangu kuwa mtambo huu utanufaisha si Stamico pekee bali pia wachimbaji wadogo, wa kati, wakubwa na sekta nzima ya madini nchini,” amesema Ghuliku.

Ameongeza kuwa, mtambo huo unahitajika sana katika kufanikisha shughuli za utafutaji wa madini, hivyo atahakikisha katika kipindi cha mwaka mmoja stamico inazalisha ipasavyo kupitia mtambo huo na hivyo kuwezesha manunuzi ya mtambo mwingine wa aina hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals