[Latest Updates]: Wadau Waitikia Wito wa Rais Dkt. Samia wa Kuongeza Thamani Madini Nchini

Tarehe : Aug. 18, 2024, 4:15 p.m.
left

●Waziri Mavunde aweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini Kinywe(Graphite)

●Zaidi ya Ajira 300 za moja kwa moja kupatikana

●Tanzania kuwa mmoja ya wazalishaji wakubwa  wa madini kinywe Afrika

●Wadau wengi waonesha nia ya kuwekeza viwanda zaidi

Kampuni ya Permanent Minerals Ltd iliyopo kijiji cha Kandaskira,Wilayani Simanjiro inaendelea na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata madini kinywe ambacho kitaongeza fursa kubwa ya kiuchumi kwa Wananchi wa Wilaya ya Simanjiro.

Akitoa maelezo mafupi,mmoja wa wamiliki wa Kiwanda hicho Ndg. God Mwanga amesema kwamba kiwanda hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani 108,000 kwa mwaka na kitatoa  ajira 300 za moja kwa moja huku Halmashauri ya Simanjiro ikitegemewa kuongeza mapato kupitia uwekezaji huo.

“Mh. Rais Dkt. Samia alielekeza juu ya uongezaji thamani madini nchini,na sasa tunaona wawekezaji na hasa wawekezaji wazawa wameanza kuitikia wito huo.

Tanzania imebarikiwa kuwa na madini haya ya kinywe katika maeneo mengi nchini ikiwemo hapa Mirerani,Simanjiro.Tutaendelea kuongeza nguvu ya utafiti ili kuvutia uwekezaji mkubwa katika eneo hilo ambalo madini maarufu hapa ni Tanzanite lakini kutokana na uhitaji mkubwa wa Madini kinywe duniani naamini uwekezaji wa kutosha pia utafanyika katika kuchimba na kuchakata madini haya.

Tanzania kwasasa ni ya tatu katika uzalishaji wa madini kinywe katika bara la Afrika,ikitanguliwa na Madagascar na Msumbiji.Tunaamini kwamba Leseni 10 zote za kati na kubwa za uchimbaji madini kinywe zikianza kufanya kazi nchi yetu itakuwa miongoni mwa nchi vinara wa uzalishaji madini kinywe Afrika”Alisema Mavunde

Akitoa salamu,Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka amepongeza uwekezaji huo mkubwa wa kiwanda na kuwasilisha kwa kiwanda maombi ya ajira kutoa kipaumbele wanajamii wanaozunguka kiwanda na pia jamii kunufaika na CSR.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mh. Fakhi Lulandala amewahakikishia wawekezaji hao ushirikiano kutoka serikalini na kutoa wito kwa wawekezaji wengi zaidi kuwekeza katika wilaya hiyo yenye utajiri wa madini mbalimbali.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals