[Latest Updates]: Leseni za Madini zaidi ya 50,000 zatolewa

Tarehe : Nov. 12, 2024, 5:38 p.m.
left

Maeneo zaidi ya wachimbaji wadogo kutengwa


TUME ya Madini imetoa jumla ya leseni za uchimbaji madini  54,626 katika kipindi cha miaka saba.

Kaimu Mkurugenzi wa Leseni na Tehama  Mhandisi Aziza Swedi amesema katika kipindi cha kuanzia 2018/2019 hadi Septemba 30, 2024, Tume ya Madini imetoa jumla ya leseni 54,626 kati ya leseni hizo, leseni za utafutaji wa Madini (Prospecting Licence-PLs) 1,683, leseni za uchimbaji wa kati (Mining Licences-MLs) 144 na leseni za uchimbaji mkubwa (Special Mining Licences-SMLs) tano.

 Aidha amesema,  leseni za uchimbaji mdogo (Primary Mining Licences-PMLs) zilizotolewa ni 35,536 leseni za uchenjuaji (Processing Licences-PCLs) 216, leseni za usafishaji Madini (Refinery Licences-RFLs) saba, leseni za uyeyushaji Madini (Smelting License’s-SLs) sita, leseni ndogo za biashara ya Madini (Brokers Licences-BLs) 12,273 na leseni kubwa za biashara ya Madini (Dealers Licences-DLs) 4,756. 

Amesema, Tume imeendelea  kutenga maeneo mahsusi kwa ajili ya  Wachimbaji Wadogo ikiwemo kuwatengenezea mazingira rafiki kwa ajili ya kupata Leseni za uchimbaji pamoja na kuwaunganisha na Taasisi za kifedha ili wapate Mikopo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji

 
“Hadi kufikia Oktoba, 2024 Tume imefanikiwa kutenga  maeneo 65 kwa ajili ya Wachimbaji wadogo katika mikoa  mbalimbali yenye shughuli za uchimbaji madini,”amesema Mhandisi Aziza.

Asema,  Tume ya Madini imeendelea kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika kuyafanyia utafiti maeneo mbalimbali  ili kuwawezesha Wachimbaji kupata taarifa za uwepo wa rasilimali madini na kufanya uchimbaji wenye tija.

Mhandisi Aziza amesema ili kuimarisha mfumo wa usimamizi wa utoaji wa leseni, Tume ya Madini  imejenga mfumo mpya  wa kuboresha uchakataji,usimamizi na utoaji wa leseni za madini.

“Baada ya  maboresho yote kukamilika itafuata hatua ya uunganishwaji wa mifumo mingine ya Serikali na uhamishaji wa data kutoka mfumo wa zamani kwenda mfumo mpya pamoja na kutoa mafunzo kwa watumiaji wa mfumo,”amesema Mhandisi Aziza.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals