[Latest Updates]: zaidi ya Milioni 900 Zakusanywa Wilayani Kakonko Katika Sekta ya Madini

Tarehe : Aug. 30, 2024, 3:44 p.m.
left

Dodoma

Imeelezwa kuwa , katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2019 hadi 2023 jumla ya shilingi 924,685,884  zilikusanywa kutokana na madini yaliyozalishwa katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.

Hayo yamesemwa leo Agosti 30, 2024 na Naibu Waziri wa Madini  Dkt. Steven Kiruswa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Aloyce John Mbunge wa Buyungu aliyetaka kujua kiasi cha fedha zilipopatikana kutokana na madini katika Wilaya ya Kakonko kuanzia Mwaka 2019 hadi 2023.

Akijibu swali , Dkt. Kiruswa amesema kuwa , Wilaya ya Kakonko ni miongoni mwa Wilaya zilizojaliwa kuwa na madini ya dhahabu nchini. 

"Kutokana na madini yanayozalishwa Kakonko Shilingi 725,171,133.52 zilitokana na mrabaha na Shilingi 199,514,750.46 zilitokana na ada ya ukaguzi wa madini yaliyozalishwa kwa kipindi kinachorejewa" amesema Dkt. Kiruswa.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameongeza  kuwa,   Madini mengine yanayopatikana katika Wilaya hiyo ni madini ujenzi aina ya mchanga , chuma, Shaba, makaa ya mawe na chokaa ambayo kwa sehemu yamechangia katika ujenzi wa barabara zinazounganisha Wilaya hiyo na maeneo mengine nchini.

Mkoa wa Kigoma umeunganishwa na wilaya nane , kakonko, kasulu, kibondo , uvinza, Buhigwe, Kusulu vijijini , Kigoma mjini na kigoma vijijini.

#InvestInTanzaniaMiningSector
 #Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals