[Latest Updates]: Waziri Kairuki, Waziri wa Maliasili China wafanya mazungumzo

Tarehe : Nov. 29, 2018, 10:06 a.m.
left

Beijing, China

Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Waziri wa Waziri wa Maliasili wa Jamhuri ya Watu wa China LU Hao Desemba 11 walifanya mazungumzo Beijing, nchini China wakati Tanzania ikishiriki katika Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini humo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimkabidhi Waziri wa Maliasili wa Jamhuri ya Watu wa China LU Hao, zawadi ya picha inayoonesha wanyama mbalimbali wanaopatikana nchini[/caption]

Waziri wa Maliasili ndiye anayesimamia masuala ya Madini nchini China.

Kufuatia mazungumzo hayo, Waziri wa Maliasili wa China aliona kuwa maombi  yaliyowasilishwa na Waziri Kairuki ni ya msingi hivyo, nchi hizo zimekubaliana kuwa na  Kundi la Pamoja  la  Kazi  kati  ya wizara hizo  mbili ambalo  litapitia na kuchambua maeneo ya ushirikiano na baadaye  nchi husika zitasainiana Mkataba wa Makubaliano.

Aidha, nchi hizo zimekubaliana kukuza ushirikiano katika maeneo ya utafiti, mafunzo na uwekezaji katika sekta ya madini.

Wizara ya Madini ilishiriki Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini tarehe 10 Desemba, mwaka huu Beijing nchini China. Jukwaa hilo liliandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals