[Latest Updates]: Wazalishaji wa Almasi Afrika Wajadili Namna ya Kuongeza Thamani Almasi Ghafi

Tarehe : March 12, 2024, 5:12 p.m.
left

Victoria Falls, Zimbabwe 

Nchi Wanachama wa Umoja wa Nchi zinazozalisha Almasi Afrika (ADPA) wamejadili namna ya kuongeza thamani Almasi ghafi pamoja na namna ya ushirikiano katika masoko ya madini hayo badala ya kutegemea masoko yaliyo nje ya Afrika pekee.

Hayo yamejadiliwa katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Tisa wa Wataalam na Baraza la Mawaziri wa ADPA unaoendelea katika mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambao umeanza leo Machi 12 na unatarajiwa kuhitimishwa Machi 14, 2024.

Akifungua Mkutano huo, Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Soda Zhemu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa ADPA, amewasisitiza Wajumbe wa Mkutano kuangalia maslahi ya pamoja kama Nchi Wanachama kwa kuimarisha ushirikiano baina yao badala ya kuchukuliana kama washindani kwenye soko.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo akiambatana na Kamishna Msaidizi wa Madini - Sehemu ya Uendelezaji Uchimbaji Mdogo ambaye pia ni Mratibu wa ADPA kwa upande wa Tanzania, Francis Mihayo pamoja na Afisa Tawala, Henry Shadolo.

Bara la Afrika likiwa na zaidi ya asilimia 60 ya Almasi ghafi duniani bado inakosa  uthabiti katika katika tasnia ya uongezaji thamani madini hayo, hivyo lengo la mkutano huo ni kutoa jukwaa la majadiliano na hatua kuhusu utambuzi wa Almasi za Afrika. 

Kuongeza thamani Almasi ghafi ndani ya bara la Afrika, itasaidia kuzuia kuuza madini hayo ambayo hayajaongezwa thamani, kwa nia ya kuongeza fursa za ajira kwa wenyeji na mapato kwa mataifa husika.

Katika Mkutano huo, baadhi ya Nchi kama Namibia, Angola, Afrika Kusini, na wenyeji Zimbabwe zimepata fursa ya kufanya mawasilisho na kuelezea mikakati ya kuimarisha tasnia ya uongezaji thamani almasi katika mataifa yao.

Hivi sasa, Zimbabwe inaongoza Mkutano wa ADPA wenye wanachama wapatao 19 ikiwa Mwenyekiti, ikisaidiwa na Sierra Leone kama Makamu wa Mwenyekiti huku Shirikisho la Urusi wakiwa waangalizi wa Mkutano huo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals