Tarehe : Aug. 2, 2018, 5:48 a.m.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema Serikali itaaendelea kusimamia ulinzi na kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite na watakaokwenda kinyume na matakwa ya Sheria, kiama chao kinakuja.
Sehemu ya wachimbaji katika eneo la Lemshuku Wilayani Simanjiro kunakofanyika shughuli za uchimbaji madini ya Green Garnet wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki hayupo pichani wakati wa ziara yake katika eneo hilo.[/caption]
Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 1 Agosti wakati wa ziara yake mkoani Manyara wakati alipotembelea migodi mbalimbali ya madini ya tanzanite ndani ya ukuta wa Mirerani.
Alisema ziara hiyo ililenga kuangalia suala zima la ulinzi katika ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, shughuli za uchimbaji madini mengine zinavyofanyika na kuangalia namna uzalishaji wa madini ya tanzanite unavyoendelea katika migodi husika.
Kairuki aliongeza kuwa, ziara hiyo ililenga kuangalia namna Sheria ya Madini inavyotekelezwa, masuala ya Mikataba ya watumishi katika migodi na namna migodi husika inavyolipa kodi mbalimbali za Serikali yakiwemo masuala ya usalama sehemu za kazi na wafanyakazi kwa ujumla.
“Utoroshaji madini hausaidii, fedha ni za haraka lakini zinawaadhibu watanzania walio wengi kwa kuwa, fedha hizo hizo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo. Hivyo, kila mtanzania awe mlizi wa mwenzake,” alisema Kairuki.
Waziri wa Madini Angellaha Kairuki akipima ubora wa madini ya Tanzanite katika kifaa maalum baada ya kuzalishwa kutoka katika mgodi wa moja ya wachimbaji madini ya tanzanite.[/caption]
Awali, akizungumza katika eneo Lemshuku kunakofanyika shughuli za uchimbaji wa madini ya Green Garnet, waziri Kairuki alisema kuwa, serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika kuchangia pato la taifa kupitia shughuli za uchimbaji, hivyo akawaasa wachimbaji nchini kufuata Sheria, kanuni na taratibu ili kufanya shughuli halali ikiwemo kulipa kodi stahiki.
Akizungmzia suala la ruzuku kwa wachimbaji wadogo, waziri Kairuki alisema hivi sasa serikali imesitisha kwa muda utoaji rukuzu kwa kuwa inaandaa utaratibu wa wazi na endelevu ambao utawezesha wachimbaji na serikali kunufaika kupitia rasilimali madini.
Aliongeza kuwa, serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za uchimbaji mdogo wa madini ikiwemo kuhakikisha kuwa inawawezesha wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati na kuongeza, “ tayari tumetenga maeneo zaidi ya 44 kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Waziri wa Madini akiteta jambo wakati alipotembelea mgodi wa Franone Mining & Gems Co. Ltd uliopo ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, Mirerani.[/caption]
Akitolea ufafanuzi suala la vibarua katika migodi ya madini, aliwataka wale wote wanaofanya vibarua katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa, wanapata mikataba yao kabla ya kuanza kazi.
Kuhusu masuala ya utoaji leseni za uchimbaji madini, Waziri Kairuki alisema ndani ya kipindi cha wiki 2 Tume ya Madini itaanza kutoa leseni kwa waombaji waliokidhi vigezo na kuongeza kuwa, kwa wanaomiliki leseni bila kuziendeleza watanyang’nywa na hivyo akawaasa wamiliki wasiokuwa na uwezo wa kuendeleza maeneo yao kutoa tarifa ili waweze kuunganishwa na wenye uwezo wa kuwekeza waweze kushirikiana.
Pia, waziri Kairuki alihamasisha kuhusu uwekezaji katika mashine za kukata na kunga’risha madini ili kuwezesha shughuli hizo kufanyika nchini na kuongeza kuwa, kupitia Sheria Mpya ya Madini hairuhusu yoyote kusafirisha madini ghafi nje ya nchi.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia madini ya Green Garnet alipotembelea moja ya migodi inayochimba madini hayo katika eneo la Lemshuku Wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara wakati wa zira yake.[/caption]
Kwa upande wake, Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mlabwa, alisema ni lazima Sheria, Kanuni na taratibu zizingatiwe wakati wa utekelezaji shughuli za uchimbaji madini na kuongeza kuwa, serikali inatambua mchango wa kila aina ya madini yanayopatikana nchini.
Naye, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Tumaini Magesa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto alisema kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo la Mirerani zinaendelea na hivyo serikali itaendelea kuboresha ulinzi na kuhakikisha kwamba unaimalika.
Imeandaliwa na:
Asteria Muhozya, Simanjiro
Afisa Habari,
Wizara ya Madini,
Kikuyu Avenue,
P.O Box 422,
40474 Dodoma,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,
BaruaPepe: info@madini.go.tz,
Tovuti: madini.go.tz
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.