[Latest Updates]: Sekta ya Madini Sehemu Sahihi ya Biashara na Uwekezaji

Tarehe : July 14, 2023, 10:43 a.m.
left

#Dkt. Kiruswa awataka Watanzania kutembelea banda la Wizara ya Madini

Dar es Salaam 

Sekta ya Madini imekuwa ni sehemu sahihi ya biashara na uwekezaji kutokana na Miongozo, Maelekezo na Maagizo mbalimbali yanayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akifungua Jukwaa la Madini Tanzania, Sabasaba Expo Village 2023 jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kiruswa amesema kuwa, Serikali itaendelea kusaidia na kuweka mazingira bora ya biashara ili kuhakikisha kuwa wawekezaji na wafanyabiashara wanafanikiwa na kuchangia katika ukuaji wa Sekta ya Madini na uchumi wetu.

Amesema, kuanzishwa kwa Jukwaa la 77 Expo Village ni ishara ya dhamira ya kukuza Sekta ya Madini na kuvutia uwekezaji nchini.

"Kupitia jukwaa hili, tunawapa fursa wadau wote walio kwenye mnyororo wa thamani ya madini kuonesha ujuzi na uwezo wao, kutafuta masoko mapya, na kujenga uhusiano na wadau wa ndani na nje ya nchi," amesema Dkt. Kiruswa.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewashukuru wadau wa Sekta ya Madini kwa kushiriki kikamilifu katika jukwaa hilo la Madini. Amesema Sekta ya Madini itaendelea kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji nchini.

Jukwa la Madini Tanzania kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya  STAMICO Meja General (Mstaafu) Michael Isamuyo, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse, Katibu Mtendaji Chemba ya Migodi Benjamini Mchwampaka na wawakilishi kampuni ya Mamba, GGM, Jitegemee Holding, ESAP Mining Service Ltd, Yaya Resources na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madin

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals