[Latest Updates]: GST Kufanya Utafiti wa Kina Kutoka Asilimia 16 hadi Kufikia 34 Ifikapo 2026

Tarehe : Feb. 26, 2025, 1:46 p.m.
left

Mpango na Bajeti ya GST kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 wapitishwa

Bodi ya GST yapitisha Mpango na Bajeti wa Taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/26

Miradi ya kimkakati ya kuongeza eneo lenye taarifa za Jiofizikia na ujenzi wa Maabara za Kanda kufanyika


Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania GST) imepitisha mpango wa bajeti ya Taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ili kutekeleza shughuli za miradi ya kimkakati  ikiwemo kufanya Utafiti wa kina wa Jiofizikia kwa njia ya kutumia Ndege ili kuongeza eneo lenye taarifa za kina za jiofizikia kutoka asilimia 16 za sasa hadi kufikisha asilimia 34 ifikapo mwaka 2026; kuboresha huduma zitolewazo na GST kwa kununua vifaa vya utafiti ikiwemo helikopta pamoja na ujenzi wa maabara ya kisasa Dodoma na maabara za kanda katika mkoa wa Mbeya na Geita.

Akizungumza katika kikao maalum cha Bodi hiyo kilichofanyika leo Februari 26 , 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Abdulkarim Mruma, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya GST CPA. Constantine Mashoko amesema Bodi imepitisha bajeti hiyo ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za GST.

Pamoja na mambo mengine, CPA Mashoko ametoa rai kwa GST kuangalia namna sahihi ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya GST Dkt. Mussa Budeba amesema Taasisi hiyo inaendelea kutekeleza majukumu yake na imejiwekea  mikakati ya kuhakikisha wanaongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Taasisi ili kufikia malengo yaliyowekwa. Aidha, amebainisha kuwa Menejimenti itaenda kutekeleza maelekezo na ushauri uliotolewa na Bodi kwa maendeleo ya Taasisi na Sekta ya Madini kwa ujumla.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals