[Latest Updates]: Serikali kujadiliana na Mgodi wa CATA Mining

Tarehe : March 28, 2018, 10:43 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa CATA Mining uliopo katika Kijiji cha Kataryo Mkoani Mara kukaa pamoja na Serikali kujadili tofauti zilizopo ili kuruhusu mgodi huo kuendelea na shughuli za uzalishaji.

Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kataryo, Elizabeth Masabu akimueleza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) kuhusu uhusiano baina ya mgodi na wananchi wakati wa mkutano wa Naibu Waziri huyo na wananchi wa Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini.[/caption]

Alitoa agizo hilo Desemba 28, 2017 kwenye mkutano na wananchi katika Kata ya Tegeruka kufuatia ombi kutoka kwa mmoja wa Wakurugenzi wa mgodi huo, Mahuza Nyakirang’ani pamoja na wananchi waliokuwa wakifanya kazi kwenye mgodi huo na wananchi wa maeneo ya jirani na mgodi waliokuwa wakinufaika na mgodi kwa namna mbalimbali la kuruhusu uzalishaji uendelee.

Alisema anatambua umuhimu wa mgodi huo kwa wamiliki na wananchi kwa ujumla na hivyo ipo haja ya kukaa pamoja kujadili tofauti zilizosababisha kusimamishwa kwa uzalishaji katika mgodi huo ili uendelee na uzalishaji.

Alisema uangaliwe uwezekano wa kuruhusu uzalishaji uendelee ili wananchi waliokuwa wameajiriwa mgodini hapo waendelee na ajira zao huku majadiliano yakiendelea kufanyika.

“Kama mlivyonieleza kuna baadhi yenu mlikua mkifanya kazi kwenye mgodi lakini tangu mgodi usimamishwe uzalishaji nanyi hamna kazi, kwahiyo ni vyema wakati mazungumzo yanaendelea na mgodi ukawa unazalisha ili waliokosa ajira warudi kazini,” alisema.

Aidha, akizungumza kwa niaba ya wananchi waishio maeneo jirani na mgodi, Elizabeth Masabu ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kataryo alimueleza Naibu Waziri Nyongo kuhusu uhusiano baina ya mgodi na wananchi na pia kumuomba kuingilia kati masuala mbalimbali ikiwemo ajira kwa wananchi wa maeneo husika, fidia, utunzaji wa mazingira na migogoro na mgodi.

Masabu aliongeza kuwa waliingia mikataba ya kirafiki na mgodi huo ambao alisema kuna makubaliano ambayo hayajafanyika na hivyo alimuomba Naibu Waziri kuwasaidia kuhakikisha mgodi huo unarejea makubaliano.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kewanja, Kata ya Kemamba Wilayani Tarime wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) akizungumzia masuala yanayohusu Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ikiwemo ulipaji wa fidia na suala la ajira kwenye mgodi huo.[/caption]

Akijibu hoja za wananchi hao, Nyongo aliuagiza mgodi kuhakikisha unaingia mkataba wa kisheria wa uwajibikaji kwa jamii (corporate social responsibility) ili Serikali ya Kijiji iweze kujipatia haki yake kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba.

Aliuagiza mgodi huo kutoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wa maeneo ya jirani kwa kazi wanazoziweza na wakati huohuo aliwaasa wananchi watakaonufaika na ajira wafanye kazi kwa uadilifu.

Kwa upande wake Nyakirang’ani alimuahidi Naibu Waziri Nyongo kwamba mgodi huo utaendelea kuboresha mahusiano na jamii na kwamba watatekeleza maagizo yake kwa wakati ikiwemo suala la ulipaji wa fidia.

Imeandaliwa na:

Mohamed Saif,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals