[Latest Updates]: Biteko ataka agizo la Waziri Mkuu litekelezwe haraka

Tarehe : April 28, 2018, 11:41 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amemwagiza Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini kumpeleka haraka Afisa Madini katika Wilaya ya Ruangwa kama alivyoagiza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Biteko aliyasema hayo tarehe 18 Januari, 2017 wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea kabla ya kuendelea na ziara yake ya kutembelea shughuli mbalimbali kuhusu Sekta ya Madini wilayani humo.

Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini Mayigi Makolobela aliyesimama, akitoa taarifa ya utekelezaji kwa naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) Wengine ni Watumishi wa Madini katika ofisi hiyo.​[/caption]

“ Teueni haraka Afisa na aende leo wakati taratibu nyingine zinakamilishwa. Suala hili lisisubiri kuhamisha ofisi. Agizo la Waziri Mkuu lazima litekelezwe haraka,”alisisitiza Biteko.

Aidha, aliwataka Watumishi wa Ofisi ya Madini Nachingwea kuwa wabunifu ili wanapofanya kazi wasitazame tu suala la kufikia malengo waliyowekewa bali pia wazingatie ubunifu.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini Mayigi Makolobela alisema hadi kufikia sasa ofisi ya Madini Mtwara imekusanya kiasi cha Shilingi 846,729,027 na Ofisi ya Nachingwea imekusanya jumla ya Shillingi 465,911,518/sawa na asilimia 93.18 na hivyo kufanya jumla ya makusanyo yote kufikia shilingi 1,312,640,545.96/ sawa na asilimia 62.51 ya lengo liliwekwa katika mwaka wa fedha 2017/18.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya kugundua kuwa Afisa Madini aliepo wilayani Nachingwea ndiye anayehudumia pia wilaya za Ruangwa na Liwale.

Imeandaliwa na:

Rhoda James, Nachingwea

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals