Tarehe : April 28, 2018, 11:50 a.m.
“Sheria mpya ya madini ya mwaka 2017 inataka kurudisha uchumi wa madini kuwa uchumi fungamanishi kwa sekta nyingine. Hatuwezi kuwa na Mgodi ndani ya nchi ambao ajira zote zinapelekwa nje ya nchi kupitia huduma mbalimbali. Unaweza kuagiza bidhaa za kila aina kutoka nje ya nchi lakini huwezi kuagiza ajira za wananchi wako zitoke nje kuja ndani, kamwe haiwezekani.”
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambapo alisisitiza viongozi kusimamia Kanuni na taratibu katika Sekta ya Madini.[/caption]
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko tarehe 3 Februari 2018, wakati akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambapo alisisitiza viongozi wa serikali katika maeneo yao kusimamia Kanuni na taratibu juu ya usimamizi wa madini.
Biteko alisema kuwa, usimamizi madhubuti wa Sheria na taratibu zilizowekwa ni sehemu imara na makini itakayowanufaisha watanzania ambapo watakuwa wamemuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amedhamiria kuhakikisha kuwa watanzania wananufaika kupitia rasilimali zao.
“Kanuni ya madini ya mwaka 2018 imeelekeza kuwa mgodi wowote unapoanza asilimia 100% za watoa huduma za chakula wanapaswa kuwa watu wa wananchi wa Tanzania, Pia huduma za ulinzi kwa asilimia 100% zinapaswa kutolewa na kampuni za ndani. Hivyo wataalamu wa sekta ya madini ni lazima kusimamia Kanuni hizo kwa usahihi,” aliongeza.
Biteko aliongeza kuwa, kampuni ya kigeni inaweza kufanya huduma hizo lakini ni lazima iingie ubia na wananchi wa Tanzania na kanuni hizi serikali imeziweka kwa makusudi kabisa ikiwa na mtazamo wa kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao.
Biteko alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho kimeingia mkataba na wananchi katika kuwatumikia kwa usimamizi madhubuti kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 hivyo, viongozi wa CCM wanapaswa kusimamia vyema serikali ili kuongeza tija katika utendaji.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza wakati wa kikao kazi na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga aakiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo.[/caption]
Aliongeza kuwa, sambamba na CCM kuisimamia vyema serikali pia aliwataka watendaji wote wa serikali kuwa na umoja katika utendaji wao kwa usimamizi madhubuti wa rasilimali madini huku akitoa onyo Kali kwa watendaji wa serikali, Viongozi, vyama vya siasa na wananchi kujihusisha na rushwa kwani kufanya hivyo ni kuzififisha juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli ya kuwainua wananchi wanyonge ili kila mtanzania aweze kunufaika na rasilimali zilizopo.
"Ndugu zangu ni aibu mno dhahabu na madini yetu mengine kuchimbwa nchini lakini yanajenga nchi nyingine, uhakika wa barabara bado hatuna katika maeneo mengi, maji bado hatuna, sekta ya afya haijaimarika, Zahanati zina shida lakini pia Karibu kila maeneo hatujajidhatiti kwa asilimia 100% Kwa hiyo Mhe Dc naomba sana msicheke na mtu yeyote anayecheza na rasilimali zetu This Must be a Serious business, Mimi najua we have the same spirit lazima tufanye kazi kwa weledi.
Pia, Naibu Waziri Biteko alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhil Nkulu sambamba na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel kwa kuimarisha juhudi na utendaji kazi katika sekta ya madini kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla huku akisisitiza kuwa kila kiongozi atapimwa kwa matokeo ya utendaji kazi wake na si kwa cheo chake.
“Waheshimiwa Viongozi, Mhe. Rais na watanzania watatupima kwa matokeo si kwa nafasi na vyeo vyetu” alisisitiza Biteko.
Na Mathias Canal, Shinyanga
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.