[Latest Updates]: Wanawake TEITI Watembelea Kituo cha Watoto Ytaima Usulini Dodoma

Tarehe : March 6, 2025, 2:56 p.m.
left

Kuelekea kilele cha siku ya kimataifa ya wanawake 2025

Dodoma

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake, leo Machi 06, 2025,  watumishi wanawake kutoka Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) wamefanya ziara ya kutembelea kituo cha watoto yatima na wenye uhitaji kilichopo Mipango jijini Dodoma.

Kituo hicho kilichopo Mipango jijini Dodoma kilianzishwa mwaka 1995, kinahudumia watoto takribani 90, wakiwemo wale wanaohitaji msaada wa malezi bora na kukabiliana na ukatilia dhidi ya watoto 

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wanawake wa TEITI, Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu, Mageni Sagenge amesema kuwa ziara  hiyo ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yenye kauli mbiu isemayo “wanawake wasichana 2025 tuimarishe haki, usawa na uwezeshaji”, itakayofanyika kitaifa tarehe 08, Machi 2025 ambapo yataadhimishwa jijini Arusha na Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan. 

Watumishi hao wanawake wa TEITI wameamua kutembelea kituo hicho na kufanya matendo ya huruma kama vile kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali  na kuwatia moyo.

“Tunatambua kila mtu ana mahitaji mbalimbali lakini nashukuru kwa michango iliyotolewa na TEITI kufanikisha jambo hili la kufanya matendo ya huruma katika kituo chetu hiki cha Usulini, jukumu la kulea watoto ni zito na linalohitaji uwajibikaji wa pamoja, hakika mnafanya kazi ya Mungu nawatia moyo japo kuna changamoto Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mama yetu Dkt. Samia Hassan Suluhu ipo pamoja nanyi kuhakikisha kuwa mnapata huduma stahiki na vituo hivi zinasonga mbele”  amesema Segenge.

Ameendelea kusema kuwa, “ Natoa wito kwa wanawake wengine kuwa sisi kama walezi tunategemewa na tuendelee kuwasaidia watanzania wenzetu wenye mahitaji zaidi lakini wanakosa msaada, ambapo kutoa ni akiba ya baadae pamoja na familia zetu.”

Awali, kwa upande wake, Mlezi Mkuu wa kituo hicho Sista Maria Peter amewashukuru wanawake wa TEITI kwa umoja huo na kusisitiza wanawake wengine kujitokeza kujitolea haswa katika kipindi hichi cha mfungo wa ramadhani na kwaresma.

Ameongeza kuwa mafanikio ya kituo hicho kimefanikiwa kulea watoto hadi kufikia hatua ya vyuo na vyuo vikuu. 

Sista Maria ameushukuru uongozi wa TEITI kwa jambo walilofanya la kuwapatia msaada na kuongeza kuwa imewatia moyo na kujiona wa thamani sana katika jamii.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals