[Latest Updates]: GGML Yaipiga Msasa STAMICO Usalama Mahala pa Kazi, Migodini

Tarehe : Oct. 10, 2024, 4:03 p.m.
left

●Yatoa mafunzo kuhusu mazingira  hatarishi kwa usalama wa wafanyakazi
● Yahimiza  kufanya kazi kwa kuzingatia  na kuacha  mazoea kazini

Shirika  la Madini  la Taifa (STAMICO) leo oktoba 9, 2024 limepata mafunzo ya usalama mahala pa kazi, hususani sehemu za migodini ili kuweza kujikinga na athari mbalimbali zinazoweza kutokea kwa mtu binafsi na wategemezi

Mafunzo haya yametolewa na wataalamu kutoka kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita Gold Mine Limited (GGML) yakilenga kuwakumbusha wafanyakazi wa STAMICO  umuhimu  wa kuzingatia matumizi ya alama za kimazingira  na vifaa kinga mahala pa kazi hususani migodini.

Akiongea  kuhusu mafunzo hayo Bw. Deusdedith Magala ameishukuru  Kampuni ya  GGML  kwa kuamua kuwafikia  na kuwapa elimu ya usalama kwa watumishi wote wa STAMICO  ili kuwajengea uelewa wa kujikinga na ajali.

Amesema mafunzo hayo yamehimiza ufanyaji kazi unaozingatia mipaka ya utendaji kazi, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kudhania ili kuepusha ajali.

Naye, Bi. Ashura Said Mratibu wa Mafunzo hayo amesema ni muhimu  kwa Shirika  kuzingatia usalama mahala pa kazi ili kuwalinda wafanyakazi  wake na athari zinazoweza kuwapata.

Amesema ni lazima  kuhakikisha  kuwepo kwa mazingira ya kazi ambayo ni salama kwa mfanyakazi kufanya kazi ili kuweza kufikia malengo kwa kuzingatia sera ya usalama mahala pa kazi

Amesisitiza kuwepo kwa mikakati ya   kukabiliana na dharura pindi inapotokea ili kuepusha athari kubwa zaidi

Amehimiza kuwepo kwa Mawasiliano kuhusu jambo au mabadiliko yoyote ya kimazingira  yanayofanyika ili kila mtu aweze kuyatambua na kuyafanyia kazi.

Kwa upande wa wafanyakazi Mohamed Kaunya ameushùkuru uongozi wa STAMICO  kwa kuandaa mafunzo  hayo ambayo  yamelenga kuwakumbusha wajibu wa kila mfanyakazi katika kuzingatia  usalama  mahali pa kazi.

Mafunzo haya ya siku mbili ya Usalama na Afya mahali pa kazi kwa wafanyakazi wote wa STAMICO yameandaliwa kwa kushirikiana na Geita Gold Mine kwa kuanzia  wafanyakazi  waliopo Dar es salaam na baadae itafanyika kwa wafanyakazi wake wote wa
Kiwira, Itumbi ( Chunya), Dodoma, Shanta, Lwamgasa, Buckreef na Katente.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals