Tarehe : July 24, 2018, 5:05 a.m.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuisaidia wizara iweze kubaini maeneo maalum ya kuzingatia yatakayowezesha kuongeza mchango wa Sekta katika Pato la Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa akiwasilisha mada ya Mchango wa Shughuli za Madini katila Pato la Taifa kwaWaziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani) na Menejimenti ya Wizara pamoja na watumishi kutoka Taasisi zake wanaofuatilia.
Aliongeza kuwa, ushauri utakaotolewa na NBS utaisaidia wizara kujipanga zaidi kuhusu namna ya kutumia fursa zilizopo katika sekta husika na sekta nyingine ili kuhakikisha kuwa pato la Sekta linaongezeka.
Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 23 Julai, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma, wakati wa kikao kati ya Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake ambapo Kaimu Mkurugenzi Takwimu za Uchumi kutoka NBS, Damian Masolwa, aliwasilisha mada kuhusu Mchango wa Shughuli za Madini katila Pato la Taifa.
Kikao hicho kinafuatia maelekezo ya Waziri Kairuki aliyoyatoa kuhusu wizara kukutana na NBS ili isaidie kuona ni namna gani wizara itaongeza mchango wake katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.
Pia, Waziri Kairuki aliwataka Watendaji wa wizara na taasisi husuan Tume ya Madini kupitia kila vifungu vya Sheria ya Madini na kuhakikisha kuwa vinatekelezwa kikamilifu.
Aidha, Waziri Kairuki alimshukuru mtaalam huyo na kuikaribisha ofisi ya NBS kuendelea kuishauri wizara kuhusu masuala ya takwimu kwa lengo la kuipeleka mbele sekta ya madini.
Wakati akiwasilisha mada, Musolwa aliishauri wizara kusimamia vizuri mianya ya mapato yatokanayo na madini pamoja na kuongeza juhudi katika kuhakikisha inapata taarifa za kutosha hususan katika madini ya ujenzi.
Pia, aliishauri wizara kuhusu kufanya tafiti za madini katika maeneo mbalimbali ya nchi jambo ambalo litaiwezesha kupata taarifa zitakazosaidia katika ukusanyaji wa mapato stahiki kutokana na shughuli za madini zinazofanyika katika sekta ikiwemo zile zinazokwenda sambamba na sekta ya madini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alimshukuru mtoa mada kutokana na elimu ya takwimu aliyoitoa na kuahidi kuufanyia kazi ushauri alioutoa.
Pia, ameitaka NBS kuendelea kutoa ushauri wa mara kwa mara wizara lengo likiwa ni kuhakikisha sekta ya madini inachangia zaidi katika pato la taifa.
Imeandaliwa na:
Asteria Muhozya, Dodoma
Afisa Habari,
Wizara ya Madini,
Kikuyu Avenue,
P.O Box 422,
40474 Dodoma,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,
BaruaPepe: info@madini.go.tz,
Tovuti: madini.go.tz
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.