[Latest Updates]: Usiku wa Madini Waupamba Mkutano wa Kimataifa

Tarehe : Oct. 26, 2023, 5:36 p.m.
left

Waziri wa Madini Malawi Apongeza Juhudi za Tanzania Kuendeleza Sekta

 
Kampuni mbalimbali Zapewa Tuzo kutambua Mchango Wao, Prof. Mruma apata Tuzo Maalum ya GeoScience

Miss Tanzania 2023 Awa Kivutio Onesho la Bidhaa za Vito na Usonara

Waziri wa Madini nchini Malawi Mhe. Monica Chang’anamuno amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi na mikakati  mbalimbali anayofanya katika kuendeleza Sekta ya Madini nchini.

Mhe. Chang'anamuno alitoa pongezi hizo Oktoba 25, 2023  katika hafla ya Usiku wa Madini uliyoambatana  na utoaji  Tuzo kwa wadau mbalimbali  wa Sekta ya Madini waliofanya vizuri ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wako kwenye maendeleo na ukuaji wa sekta.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe.Chang’anamuno alisema kuwa mazingira halisi yanaonesha kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea kufanya juhudi nyingi sana katika kuendeleza Sekta ya Madini kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Serikali.

Akielezea kuhusu Mpango wa Wajibu wa Migodi kwa Jamii inayozunguka Mgodi (CSR) , Mhe. Chang’amuno aliipongeza kwa kuwepo Mpango mzuri unaounganishwa na Sera ya Madini katika kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania kushiriki katika uchumi wa madini.


Mhe.Chang'anamuno aliongeza kuwa amejifunza mengi kuhusu shughuli za uongezaji na kueleza kuwa ataishauri Serikali ya Malawi kuhusu kuwepo wa Kituo cha mfano katika utoaji  mafunzo ya uongezaji uhamani nchini Malawi kama ilivyo kwa Kituo cha Uongezaji Thamani Madini  Tanzania cha TGC.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Anglo Ashanti kampuni iliyokuwa mdhamini Mkuu  wa hafla ya Usiku wa Madini Terry Strong, akitoa hotuba fupi alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa maendeleo ya sekta ya madini.

Katika usiku huo zilipata tuzo kupitia  vipengele mbalimbali ikiwemo  Utunzaji wa Mazingira Migodi,  Tuzo ya  Ukataji na Uongezaji Thamani Madini,  Ulipaji wa Mapato ya Serikali, Uwezeshaji wa Ushiriki wa  Wananchi katika Sekta ya Madini, Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii zinazozunguka Migodi,  Mwanamke bora katika uchimbaji wa madini , Mshindi Bora katika Kujenga na  tiuzo maalum   kwa mtaalam aliyetoa mchangomkubwa katika sekta ya madini ambapo Kamishna wa Tume ya Madini Prof. AbdulKarim Mruma alipata tuzo kama Mtaalam wa Geoscience  katika ukuzaji wa sekta ya madini na maendeleo  ya nchi.

 Kampuni zilizoshinda katika usiku huo kupitia ushindi mbalimbali ni pamoja na Twiga Minerals Corporation, Shanta Gold, Ako Group, GGML,Appex resources, Ruvuma Coal Limited, Jitegemee Holding, The Tanzanite Experience na Leminatha Colonel  Kabigumila.

Wakati huo, huo, Miss Tanzania Mwaka 2023 Halima Kopwe alikuwa kivutio katika hafla ya Usiku wa Madini wakati wa Onesho la Vito na bidhaa za mapambo ambapo pamoja na warembo wengine walipata fursa ya kupita jukwaani kuonesha bidhaa za madini ya vito na usonara kutokana na madini mbalimbali yanayozalishwa na bidhaa mbalimbali za vito na usonara zinazotengenezwa   na kampuni za ndani.

Kampuni zilizoonesha madini yake ni pamoja na  Gem Point, Gem Tanzanite,Ruvu Gemstone, Tanzania Gemological Centre (TGC) na Facet Gems

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals