Tarehe : Jan. 14, 2019, 10:41 a.m.
Kufuatia kukaidi Wito wa kuonana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela kutokana na kufanya ununuzi haramu wa madini ya dhahabu ikiwemo kufadhili uchimbaji haramu, Naibu Waziri Nyongo amevitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Iringa kuwakamata Mansoor Almasi na Jacob Mwapinga iwapo watashindwa kuripoti wenyewe katika Mamlaka zinazohusika.
Naibu Waziri wa Madini Stansaus Nyongo akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua mgodi wa Nyakavangala. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.[/caption]
Naibu Waziri Nyongo ametoa agizo la kukamatwa wahusika hao baada ya kukiuka agizo la kuonana na viongozi hao kwa hiari ambapo walielekezwa kuonana na Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa Januari 15.
Pia, kabla ya wito wa Naibu Waziri, awali, wahusika hao walitakiwa kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa wakiwemo Maafisa Madini kwa ajili ya kuupatia suluhisho mgogoro huo katika mgodi wa dhahabu wa Ulata, kijiji cha Ulata wilaya ya Iringa unaomilikiwa na Ibrahimu Msigwa.
Naibu Waziri Nyongo alibaini kuwa Mansoor na Mwapinga wanafanya ununuzi wa madini kinyume cha Sheria ikiwemo kufadhili shughuli za uchimbaji katika mgodi ambao siyo wamiliki wake.
Pia, Naibu Waziri ameelekeza baada ya wahusika hao kukamatwa wanatakiwa kutoa maelezo kueleza ni lini watalipa kodi wanazodaiwa na serikali baada ya kufanya shughuli hizo bila kulipa kodi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wachimbaji hao, Naibu Waziri Nyongo aliwaeleza kuwa, Serikali inamtambua Ibrahimu Msigwa kama mmiliki halali baada ya kuwa na vibali vya kumiliki leseni ya mgodi huo na hivyo kutoa wito wa kuonana na pande zote ili kuhakikisha kuwa anatoa suluhisho la mgogoro uliopo baina ya Msigwa, Mansoor, Mwapinga na wachimbaji.
Akihitimisha ziara yake mkoani Iringa Januari 15, Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi katika migodi ya Ulata na Nyakavangala.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimwonesha jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua migodi ya Nyakavangala.[/caption]
Amesema wamiliki wa leseni wanaotumia mrabaha kwa ajili ya kufanya masuala mengine ya kijamii wanakiuka taratibu na kueleza kuwa, fedha za kufanyia shughuli za maendeleo zinapaswa kutoka katika fedha za Uwajibikaji kwa jamii ambazo halmashauri zinapanga kupitia Baraza la Madiwani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema wahisika Mwapinga na Almasi wana kiburi na kwamba waliitwa kwa ajili ya kuongea ili ku[ata fursa ya kujieleza na a kueleza ni lini watalipa mrabaha lakini wamekaidi hivyo kinachofuatia ni wahusika kukamatwa.
Naibu Waziri Nyongo alifanya ziaea katka mgodi wa Ulata Janauri 14 akilenga kukagua shughuli za uchimbaji madini katika mgodi huo ikiwemo kutatua mgogoro uliokuwep katika mgodi huo baina ya mmiliki halali Ibrahimu Msingwa, wanunuzi haramu wa madini hayo Mansoor Almasi na Jacob Mwapinga.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.