[Latest Updates]: Profesa Msanjila Akutana na Kampuni ya Madini ya Twiga

Tarehe : Oct. 1, 2020, 11:15 a.m.
left

Leo tarehe 01 Oktoba, 2020 Katibu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amekutana na watendaji wa Kampuni ya  Madini ya Twiga jijini Dodoma kwa ajili ya kupata taarifa  ya utekelezaji wa kampuni hiyo pamoja na changamoto zake kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.

Wengine waliohudhuria katika kiko hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Kamishna wa Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Kamishna Msaidizi- Ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini kutoka Wizara ya Madini, Terace Ngole na watendaji wengine kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji wa kampuni hiyo, Profesa Msanjila ameitaka kampuni ya Twiga kuhakikisha inatoa kipaumbele cha ajira kwa watanzania wenye sifa kama Sera ya Ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini inavyotaka.

“Ni vyema mkahakikisha ajira ambazo watanzania wenye sifa wanaweza kupata zinatolewa, badala ya kutoa ajira kwa wageni pekee,” amesema Profesa Msanjila.

Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila ameitaka kampuni ya Twiga kuhakikisha inatangaza mpango wa manunuzi wa mwaka katika vyombo vya habari kama vile magazeti na tovuti mbalimbali ili kutoa fursa kwa watanzania wengi kujipanga na kuomba zabuni za kutoa huduma kwenye kampuni hiyo.

Aidha, Profesa Msanjila ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa viwango vya mishahara kulingana na sifa na uzoefu wa wataalam wa Tanzania na wa kutoka nje badala ya kuwepo na utofauti kulingana na uraia.

Awali akielezea utendaji wa kampuni hiyo Meneja wake, Benedict Busunzu ameeleza kuwa katika shughuli zake za kila siku kampuni imekuwa ikishirikisha jamii inayozunguka mgodi wake fursa za biashara na kununua bidhaa mbalimbali kutoka katika jamii husika.

Ameongeza kuwa, kampuni inaendelea kubuni teknolojia mbalimbali ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji wa madini zinaleta tija huku wakizingatia usalama wa afya na mazingira.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals