Tarehe : March 26, 2019, 2:55 p.m.
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd, ya Marekani, Rocky Smith na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield ofisini kwake Jijini Dodoma.
Watendaji hao wapo nchini kwa ziara ya kawaida ya kikazi ya siku tano ambapo waliomba kukutana na Waziri wa Madini.
Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo inakusudia kuwasilisha taarifa juu ya hali na Maendeleo ya soko la dunia kwa Madini ya Rare Earth Elements na kuzungumzia hatua iliyofikiwa kwa ombi la leseni ya uchimbaji Mkubwa wa madini hayo.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amesema wizara iko tayari kuipokea kampuni husika nchini baada ya kukamilika kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu Rocky Smith, amesema kuwa, amefurahishwa na ushirikiano unaooneshwa na wizara na kuahidi kuanza shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa taratibu
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.