Tarehe : Oct. 19, 2023, 8:34 a.m.
# Utoroshaji Madini kunaikosesha Serikali Mapato
# Aeleza zaidi ya Kilogram 4 za madini zilikamatwa Kahama
Serikali imewataka wadau wote wa sekta ya Madini nchini kutojihusisha na vitendo vya utoroshaji madini katika maeneo yoyote yenye uchimbaji, uhifadhi na Uuzaji kwani kwa kufanya hivyo kunaikosesha Serikali kupata mapato yatokanayo na rasilimali madini.
Hayo yamebainishwa leo tarehe Oktoba 19 , 2023 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akizungumza na Wanachama wa Chama cha Mabroka Tanzania (CHAMMATA) jijini Dodoma.
Mhe.Mavunde amesema kuwa Serikali ina mipango mingi katika kuendeleza sekta ya Madini lengo ikiwa ifikapo mwaka 2025 sekta hii kuchangia asilimia zaidi y kumi (10%) katika pato la Taifa (GDP) kama mpango wa Maendeleo wa Dira ya Taifa 2025 unavyoelekeza.
Akielezea kuhusu mchango wa Madini katika Pato laTaifa Mhe.Mavunde alifafanua kuwa katika Mwaka 2022/2023 sekta ya Madini ilikusanya zaidi ya bilioni Mia sita huku asilimia 40 ikichangiwa na wachimbaji wadogo , wafanyabiashara wa madini wa ndani na Broka.
Akielezea kuhusu mzunguko wa fedha katika mnyororo mzima wa sekta ya madini , Mhe.Mavude amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliweza kukusanya mapato ya kodi ya ndani kiasi cha Trilioni mbili hii ni kulingana na mzunguko wa pesa katika masoko ya ndani ya madini.
Naye , Mwenyekiti wa chama cha CHAMMATA Jeremia Kituyo ameshauri kuwa ili kuondokana na utoroshaji wa madini nchini ni vyema Serikali ikaja na mpango wa kukate leseni kwa mfumo wa kikanda hiyo itatoa wigo mpana kwa wafanyabiashara kutoka kanda moja na nyingine.
Kituyo aliongeza kuwa ni muda muafaka sasa serikali ikaiweka biashara ya madini kuwa biashara huria katika masoko ya madini hususani katika minada hii itawezesha bei kuwa shindani katika masoko ya madini.
Akielezea kuhusu lengo la kuanzishwa kwa CHAMMATA Kituyo alifafanua kuwa lengo ni kuwaunganisha wafanyabiashara wa madini na Serikali pamoja na kutetea na kusimamia haki za wafanyabiashara wa madini nchini.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.