[Latest Updates]: Zaidi ya Trilioni 1.8 Zachangiwa na Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania

Tarehe : Sept. 12, 2024, 1:19 p.m.
left

Dar es salaam

Imeelezwa kwamba zaidi ya shilingi trilioni 1.8 zilichangiwa na Kampuni zinazojishughulisha na sekta ya Uziduaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini.

Hayo yalibainishwa na waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati wa akizindua ripoti ya 14 ya Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa Mwaka wa Fedha wa 2021/22.

Waziri Mavunde alisema kuwa ripoti hiyo inaonyesha mchango wa sekta hizo kwa jamii ambapo amewataka wadau wa maendeleo  kutumia takwimu zilizopo katika ripoti hiyo katika mijadala, warsha na makongamano mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi hususani katika sekta husika.

Akielezea kuhusu ulinganisho wa mapato kutoka katika Kampuni, Waziri Mavunde alieleza kwamba ripoti hiyo inaonesha ulinganisho wa mapato kutoka katika kampuni 44, ambapo  Kampuni 26 za Madini, Kampuni 7 za Gesi Asilia na Kampuni 11 za Utoaji huduma kwenye mnyororo mzima wa thamani Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

Akifafanua kuhusu mafanikio ya  Mpango wa Ushirikishwaji wa Jamii katika utoaji huduma migodini, Waziri Mavunde ameeleza kuwa katika Mwaka wa Fedha  2023/24  kiasi cha shilingi trilioni 3.1 zilitumika kwenye manunuzi ya bidhaa na utoaji huduma katika sekta ya Madini.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dkt. Mathayo David Mathayo aliipongeza kamati ya TEITI kwa kazi nzuri ikiwa pamoja na kuweka kipaumbele cha Uwazi na Uwajibikaji kwenye mapato yatokanayo na Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa manufaa ya Taifa.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo, alipongeza TEITI kuwa Taasisi rasmi inayojisimamia katika masuala ya Uziduaji ambapo kupitia ripoti zake inajibu maswali mbalimbali kwa jamii na wadau husika  yanayohusiana na Uziduaji kwenye sekta ya Madini , Mafuta na Gesi Asilia.

Awali, akielezea kuhusu  mwenendo wa utoaji ripoti na mafanikio yake , Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI Ludovick Utouh amesema kuwa,  mwezi Novemba 2023, Bodi ya EITI iliwasilisha ripoti ya kuonesha kuwa Tanzania  imeingia daraja la tatu kwenye kutekeleza viwango vya Kimataifa kutoka katika taasisi ya EITI.

Utouh aliongeza kuwa, kwenye viwango vya upimaji vya  EITI kwa  mwaka 2019, TEIT ilipata asilimia 82.5 kwenye ushirikishwaji wa wadau na  asilimia 73.5 kwenye Uwazi.

Akielezea majukumu ya TEITI, Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI Mariam Mgaya alisema, TEITI ina majukumu mbalimbali lakini moja ya jukumu lake kubwa ni kuhakiki na kuwasilisha ripoti ya Uwajibikaji wa Kampuni katika ulipaji wa mapato na kodi kwa Kampuni za Uziduaji katika sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals