[Latest Updates]: Rasmi Vijana Kupatiwa Fursa Sekta ya Madini

Tarehe : Sept. 28, 2023, 8:20 a.m.
left

• Waziri Mavunde Aainisha Programu ya MBT

• Itashirikisha vijana kwa asilimia 100

• Asilimia 70 ya fedha za migodi ni manunuzi

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanisha Programu ya Mining for Better Tommorrow ( MBT) itakayo wawezesha vijana kushirikishwa katika sekta ya Madini kwa kujengewa uwezo na kupatiwa mitaji , vifaa na mashine ili wachimbe madini kwa uhakika bila kupoteza mitaji.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 28,2023 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde katika kongamano la Mpango wa Ushirikishwaji Wananchi kwenye Sekta ya Madini (local content) lililofanyika Viwanja vya EPZ Mkoani Geita.

Akielezea kuhusu programu ya MBT , Mhe. Mavunde amesema hivi sasa nguvu kazi kubwa ipo kwa vijana hivyo ni vema vijana wengi wa kitanzania wakishiriki katika sekta ya madini kupitia programu ya MBT ambayo itasimamiwa na Serikali.

Waziri Mavunde amefafanua kuwa MBT itawajengea uwezo vijana kwa kuwapatia mitaji na kuwaunganisha katika Taasisi za  fedha , kuwapatia wataalam waliopo katika sekta  ili wapate ushauri elekezi katika hatua za Utafutaji , Uchimbaji , Uchenjuaji na Uthaminishaji .

Aidha , Mhe. Mavunde ameongeza kuwa Sheria ya Madini Sura 123 , Kifungu cha 102 kinataka Kampuni za uchimbaji madini kutoa kipaumbele kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa na Watanzania.

Amesisitiza kuwa kifungu hicho kinaendana na Matakwa ya Kanuni za Ushirikishwaji ambazo zilitungwa mwaka 2018 na kufanyiwa marekebisho 2019 na 2022.

Akizungumzia kuhusu mpango wa manunuzi kutoka katika migodi mikubwa, Mhe. Mavunde amesema zaidi ya  asilimia 70 ya fedha za migodi zinapelekwa katika mpango wa manunuzi, hivyo kuna haja ya kufanya tathmini ni namna gani watanzania watafaidika na fedha hizo.

Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mkuu wa Mkoa wa  Geita , Naibu Gavana wa BoT, Mbunge wa Geita Mjini , Mkuu wa Wilaya ya Chunya , Mwenyekiti wa Tume ya Madini , Kamishna wa Madini , Wakuu wa Taasisi za Umma , Viongozi wa Vyama vya Wachimbaji wadogo , Wawakilishi wa Migodi mikubwa na Kati , wadau wa Sekta ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals