Tarehe : Dec. 18, 2018, 10:11 a.m.
Na Rhoda James, Mahenge
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameufungua mgodi wa Wachimbaji Wadogo wa Mahenge baada ya kufungwa kwa takribani miezi Mitano tangu Julai 10, 2018.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akikata utepe kuashiria uziduzi wa Ofisi ya Madini Wilayani Ulanga katika Mji wa Mahenge uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2018.[/caption]
Mgodi huo wa madini ya Vito aina ya Spino uliopo Wilayani Ulanga ulisimamishwa kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchimbaji wa madini ikiwemo kutolipa kodi za Serikali.
Akizungumza katika mkutano kati yake na wachimbaji Biteko alisema kuwa, Sekta ya Madini haipo kwa ajili ya kufunga migodi, na kuongeza kuwa, hakuna mchimbaji yeyote atakayeruhusiwa kuchimba katika eneo hilo hadi pale atakapokuwa amelipa madeni yake angalau ya awamu ya kwanza.
Pia, alisema kuwa, ikiwa kuna mchimbaji ambaye atakiuka taratibu za uchimbaji, atachukuliwa hatua za kisheria na si kwa kufungiwa mgodi tu bali atapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
“Nyie ni wadau muhimu katika sekta ya maendeleo, na mkilipa kodi, ikaonekana imefanya nini, hata wawekezaji hawatakwepa kulipa kodi,” alisema Biteko.
Aliwataka Wachimbaji Wadogo wa Mahenge kubadilika na kufuata taratibu zilizowekwa kisheria na kusema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano haitaki rushwa hususan kwenye Sekta ya Madini.
Aidha, pamoja na kufuungua mgodi huo, Biteko pia alizidua Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mahenge, ikiwa ni mojawapo ya mahitaji ya awali ili shughuli za uchimbaji madini katika Mji wa Mahenge ziende kama inavyotakiwa.
Pia, Biteko alimtaka Afisa Mkazi wa Mahenge, Tandu Jirabi kuhakikisha leseni za dealers zinasainiwa ili pamoja na kutoa utaratibu kwa wadau hao kuhusu namna ambavyo wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kabla ya kupatiwa leseni.
Mbunge wa Jimbo la Mahenge Goodluck Mlinga akiwahutubia wananchi pamoja na wachimbaji wadogo wa madini (hawapo pichani) wilayani Ulanga katika mji wa Mahenge, wakati wa ziara ya Naibu Waziri Biteko.[/caption]
“Mzawa lazima awe na mashinetano na mwekezaji kuwa na mashine 30,” alisema Biteko.
Aidha, Biteko alitoa wito kwa viongozi wa Halmashauri ya Mahenge kuhakikisha kuwa fedha zinazolipwa kama kodi zinatumika ipasavyo katika kuwezesha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo kujenga Zahanati, Shule, Barabara na kadhalika.
Kwa Upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mahenge Goodluck Mlinga alimshukuru Naibu Waziri Biteko kwa kufugua mgodi huo wa wachimbaji wadogo na kuwataka wananchi wa Mahenge kufuata taratibu zinazotakiwa ili kuepusha usubufu kama huo uliojitokeza hapo awali.
Mlinga alisisitiza kuwa, kodi inayolipwa na Wachimbaji Wadogo lazima itekeleze majukumu yaliyopangwa na kumwakikishia Naibu Waziri kuwa wachimbaji watalipa kodi kwa kishindo.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema kuwa Rais Magufuli anataka kila mwananchi afaidike na rasilimali za madini, hivyo, kuwataka wananchi na Wachimbaji wote wa Mahenge kufuata taratibu zilizopo ili kila mmoja wao afaidike na rasilimali hiyo.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.