[Latest Updates]: Uganda Yafurahishwa Utendaji Kazi Maabara ya GST na Masoko ya Madini

Tarehe : Dec. 4, 2024, 10:47 a.m.
left

Waipongeza GST kufikisha  miaka 100 mwaka 2025

Wafurahishwa GST kuwa na Ithibati za uchunguzi wa madini

Wafurahishwa na mtandao wa masoko ya madini nchini

Na.Samwel Mtuwa - Dodoma

Ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Ujumbe maalum kutoka Wizara ya Nishati na Idara ya Maendeleo ya Madini nchini Uganda, ujumbe huo umefurahishwa na mifumo ya utendaji kazi ya Upimaji na Utambuzi wa sampuli za madini  na miamba katika maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo , Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda Mhandisi Irene Bateebe amesema kuwa kulingana na mifumo iliyopo hususan katika mpangilio kuanzia upokeaji wa sampuli za miamba na madini mpaka kwenye hatua ya utambuzi  tumejifunza mengi na imekuwa faraja kwetu kwa sababu tulichokiona ni maendeleo makubwa.

Mhandisi Bateebe amefafanua kuwa nchini Uganda wanayo taasisi inayojiuhusisha na upimaji na tafiti za jiosayansi ambayo inaitwa Uganda Geological Survey (UGS) lakini kwa upande wa Maabara Tanzania imepiga hatua.

Akielezea kuhusu mada ya upatikanaji wa  Ithibati ya kimataifa kwa maabara , Mhandisi Bateebe ameeleza kuwa Maabara ya UGS bado haijapata Ithibati katika Elementi yoyote ya madini lakini kupitia ziara hii tumepata uelewa mpana wa namna ya kuandaa taarifa na nyaraka sahihi ili kupata ithibati.

Kwa upande wa masoko ya madini, Mhandisi Bateebe  amefurahishwa na mifumo ya masoko kwa jinsi inavyofanya kazi pamoja kuweza kutambua uhalisia wa madini yanayopelekwa sokoni ikiwa pamoja na wingi wa idadi ya masoko yanayofanya biashara ya madini nchini.

Awali, akiwakaribisha katika ofisi za  GST , Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba ameuelezea ujumbe huo kuhusu mikakati mbalimbali iliyopo ya kuongeza idadi ya uchunguzi wa sampuli katika elementi za madini mkakati na madini adimu ikiwa ni mpango maalum wa kisekta kupitia maabara za GST.

Naye , Mratibu wa Mipango ya Maendeleo  kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Uganda ,Bi. Hope Kyarisiima ameipongeza Tanzania kwa kuweka misingi imara katika mnyororo wa thamani madini ambao unalenga kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo ili kuondokana na umasikini pamoja na uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wake , Mkuu wa kitengo cha Miradi na Utafiti kutoka taasisi ya Chemba ya Migodi nchini Uganda Kenneth Asiimwe , amesema kuwa Sekta ya Madini nchini Tanzania imepiga hatua kubwa hususan katika ushirikishwaji wa wachimbaji wadogo kwenye maeneo mbalimbali kama mada za GST na STAMICO zilivyoonesha wakati wa kikao.

Asiimwe ameongeza kuwa wachimbaji wadogo ni muhimu sana katika kuendeleza sekta ya madini , kwasababu wanachimba kwa mfumo endelevu hivyo juhudi ziendelee kuwajengea uwezo  kwa maendeleo ya taifa.

Pamoja na mambo mengine, ujumbe huo umepata fursa ya kutembelea masoko ya madini mkoani Dodoma ili kujionea biashara ya madini inavyofanyika katika  masoko .

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals