[Latest Updates]: Waziri Mavunde Akaribisha Sekta Binafsi Kushirikiana na serikali Kwenye Utafiti wa Madini

Tarehe : March 4, 2025, 2:40 p.m.
left

Awasilisha mpango wa Mining Vision 2030

Serikali yajipanga kuongeza eneo kubwa zaidi lililofanyiea Utafiti wa Madini wa kina

Kampuni za Utafiti Madini zakaribishwa Tanzania

Aelekeza STAMICO kufanikisha upatikanaji wa vifaa ya Utafiti wa awali  kwa ajili ya wachimbaji wadogo

Toronto, Canada

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amezikaribisha nchini Tanzania Kampuni za Utafiti wa madini kushirikiana na serikali katika kutimiza malengo ya Mining VISION2030 ambayo imejikita katika kufanya utafiti wa kina wa madini kufikia eneo la ukubwa wa asilimia 50 kufikia mwaka 2030.

Mh. Mavunde ameyasema hayo jana Toronto,Canada wakati akihutubia kikao cha Mawaziri wa Madini kutoka nchi mbalimbali duniani,Kampuni za Utafiti na Uendelezaji Migodi na Asasi za kiraia.

“Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia S. Hassan imeweka mazingira wezeshi ya kiuwekezaji,hivyo ni fursa kubwa ya Kampuni za Utafiti kuja kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mkakati wake wa kuongeza eneo lililofanyiwa utafiti wa kina wa madini.

Kwa sasa Serikali kupitia Wizara ya Madini,inatekeleza mpango wa utafiti wa madini wa kina kutoka eneo la utafiti wa kina la asilimia 16 kufikia eneo la asilimia 50 kufikia mwaka 2030.

Kwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani,uongozi imara na mazingira mazuri ya kiuwekezaji nichukue fursa hii kuwakaribisha wadau kuungana na serikali katika mpango wake huu wa utafiti wa kina wa madini nchini kwa kuwa serikali peke yake haiwezi kufanya kwa eneo lote hivyo sekta binafsi ni muhimu katika kufikia azma“Alisema Mavunde

Awali akiwa katika mabanda ya maonesho ya vifaa vya Madini,akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mh. Joseph Sokoine na wataalamu wa Wizara ya Madini,Waziri Mavunde amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse kuangalia namna ya upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa awali wa madini ili wakati wachimbaji wadogo wakipata huduma ya uchorongaji kuwepo pia vifaa vya awali vya kusaidia kuonesha maeneo yanayopaswa kuchorongwa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals