[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa Aupongeza Mkoa wa Singida Kuvuka Lengo Ukusanyaji Maduhuli

Tarehe : July 11, 2024, 3:30 p.m.
left

Singida

Naibu Waziri wa Madini,Dkt. Steven Kiruswa ameupongeza mkoa wa Singida kwa kuvuka lengo  walilopangiwa kukusanya kwa asilimia 145.

Dkt.Kiruswa  alibainisha hayo  Julai 10, 2024 katika ziara yake ya kikazi kwa wachimbaji wadogo wa madini inayoambatana na ukaguzi wa  miradi ya kimkakati inayosimamiwa na  mgodi wa kati wa uchimbaji dhahabu wa Singida Gold Mine pamoja na  kupokea taarifa juu ya uwajibikaji wa mgodi kwa Jamii inayozunguka mgodi huo (CSR).

Akizungumza baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Afisa Madini Mkazi mkoa wa Singida Mha. Sabai Nyansiri , Dkt. Kiruswa alisema kuwa awali mkoa wa Singida ulipewa lengo la makusanyo TZS 12bilioni lakini hadi kufunga mwaka wa fedha 2023/24 Ofisi hiyo ilikuwa imekusanya 18bilioni.  Hii ni kutokana na juhudi zilizowekwa na huu ni mfano wa kuigwa.

Pia , Dkt.Kiruswa aliupongeza Mgodi huo kwa utekelezaji wa Mpango wa Wajibu wa Mgodi kwa Jamii inayozunguka mgodi kwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa nyumba za jamii , madarasa ya shule na kuweka mifumo mizuri ya utunzaji mazingira katika eneo la mgodi.

Kwa upande wake , Mkuu wa  wilaya ya Ikungi Thomas Apson aliishukuru wizara ya madini kupitia miradi ya kimkakati katika wilaya ya Ikungi na aliomba wizara kuendelea na utafiti wa madini ili kugundua maeneo mapya ya madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili wachimbe kwa uhakika bila kuleta migogoro .

Katika ziara hiyo Dkt.Kiruswa aliambatana na wataalam kutoka Wizara ya Madini , Tume ya Madini , viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals