[Latest Updates]: Uendelezaji wa Mradi wa Kabanga Nickel Waungwa Mkono na Wadau Mbalimbali Kimataifa

Tarehe : Aug. 27, 2024, 3:32 p.m.
left

-Serikali ya Marekani yaunga mkono uongezaji thamani madini ya Nickel Nchini

-Falsafa ya 4R ya Rais Samia yavutia uwekezaji nchini

-Waziri Mavunde akutana na ujumbe mzito wa Kampuni ya BHP juu ya uendelezaji wa mradi wa Kabanga Nickel

-Kiwanda cha kusafisha madini cha zaidi ya Dola Milioni 500 kujengwa Kahama

Dar es salaam

Serikali ya Marekani imesisitiza nia ya kushiriki katika kuendeleza Mradi wa Kabanga Nickel na Kampuni ya BHP imeweka  mkazo wa ushiriki wake katika Mradi huo ambao ni kati ya miradi mikubwa na kielelezo katika sekta ya madini nchini ambapo utekelezaji wa Mradi huu wa Madini Mkakati ni muhimu kwa wakati huu ambapo madini haya yanayohitajika sana duniani hususan  kwa ajili ya mageuzi ya nishati. 

Hayo yamesemwa Agosti 26, 2024 katika mazungumzo kati ya Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde na kampuni ya Tembo Nickel ambayo Serikali ya Tanzania ni Mbia ili kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Kampuni mama ya Tembo Nickel pamoja na Serikali ya Marekani kupitia kwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Balozi Battle na Ujumbe wa Marekani ulioongozwa na Bi.Helaina Matza, Mratibu Maalum wa Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa Ajili ya Mpango maalum wa Nchi Saba Zilizoendelea Zaidi Kiuchumi Duniani G7.

Katika ujumbe huo uliowasilishwa ma Bi.Matza ulibeba malengo ya  kuwezesha miradi mbalimbali ya kimkakati (PGII) na pia unathibitisha kuwa nchi ya Tanzania ni nchi inayovutia wawekezaji na mazingira ya uwekezaji ni rafiki na hii imechochewa sana falasafa ya uongozi wa Mh Rais Dkt.Samia S. Hassan ya 4R-Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reform (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga upya).

Akizungumza katika mkutano huo Waziri Mavunde ametoa shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha zaidi uhusiano na Marekani ambao ndio umeleta mafanikio haya. 

Mafanikio haya yanatokana na mikakati ya Mhe. Rais katika mashauriano yake kwenye Mkutano wa Marekani na Afrika uliofanyika mwaka 2022 na pia ujio wa Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris wakati wa ziara yake Tanzania mwezi Machi 2023.

Waziri Mavunde alipata wasaa wa kukutana na Afisa Mkuu wa Maendelezo wa Kampuni ya BHP Bi. Catherine Raw aliyekuja nchini kutizama maendeleo ya Mradi wa Kabanga Nickel na kuisisitizia Serikali ya Tanzania nia ya kushiriki katika kuendelea Mradi huu ambao unaenda sambamba na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha madini kitakachojengwa Wilayani Kahama,Mkoa wa Shinyanga uwekezaji utakaogharimu zaidi ya Dola Milioni 500.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals