[Latest Updates]: Upekee wa Jiolojia ya Tanzania Wahamasisha Washiriki Mkutano wa Madini Muhimu Afrika

Tarehe : Nov. 9, 2024, 5:36 p.m.
left

Utekelezaji Vision 2030 wawa chachu ya uwekezaji

Capetown

Imeelezwa kuwa Jiolojia ya kipekee ya Tanzania inadhihirishwa na uwepo wa Madini ya Tanzanite ambayo hayapatikani kwingine popote duniani huku yakitajwa kuwa ni madini adimu mara Mia ya madini ya almasi na adimu mara Elfu Moja kwa madini mengine ya Vito.

Hayo yalielezwa Novemba 6, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse wakati akitoa wasilisho kuhusu Hali ya Sekta Nchini (country mining sector sport light)  katika Kilele cha Mkutano wa Madini Muhimu Afrika uliofanyika Cape Town, Afrika Kusini, Dkt. Mwasse aliongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki katika mkutano huo.

Alisema kuwa, upekee huo umeifanya Tanzania mbali na madini hayo, inazo aina zote za madini yanayopatikana duniani ikiwa ni pamoja na madini muhimu yanayohiyajika kwa ajili ya nishati safi. 

Aliongeza kwamba, ili Tanzania iweze kunufaika na madini hayo, imeandaa mkakati wa Madini Vision2030 wenye lengo la kupunguza uwekekano wa wawekezaji kupata hasara kwa kufanya tafiti maeneo ambayo hayana taarifa za kijilojia (derisking the sector).

‘’Mkakati huo unalenga kufanya utafutaji wa madini kwa njia ya ndege (High Resolution Airbone Survey) kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030 kutoka asilimia 16 ya sasa, jambo litakalo saidia kupata taarifa za uwepo wa madini ikiwemo madini muhimu. Alieleza kuwa hii itavutia wawekezaji wengi kwani watakuwa wanafahamu madini yapi yanapatiaka wapi,’’ alisisitiza Dkt. Mwasse.

Mbali na makakati huo, mikakati mingine aliyoeleza ni pamoja na kuendeleza na kuimarisha miundombinu ya barabara, reli, bandari na ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu nyerere na kusema, ‘’kukamilika kwa bwawa hilo ambalo linazalisha nishati safi isiyochangia mabadiliko ya tabianchi lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 litakuwa mkombozi kwa baadhi ya nchi Jirani zenye uhitaji wa umeme,’’. Aliongeza Dkt. Mwasse.

Kutokana na usimamiazi mzuri wa uchimbaji mdogo nchini, Tanzania ilitajwa kuwa ni nchi yam fano kwa nchi ya Afrika kujifunza namna ya kuwasimamia wachimbaji hao ili waweze kunufaika na rasilimali zilizopo katika nchi zao.

#TMIC2024

#InvestInTanzaniaMiningSector

#ValueAdditionforSocioEconomicDevelopment

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals