[Latest Updates]: Vilio na huzuni vyatawala tena mgodi wa Imalanguza

Tarehe : Nov. 10, 2019, 7:41 a.m.
left

Na Issa Mtuwa “WM” - Geita

Majonzi na huzuni vimetawala kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo wa Imalanguza wilaya ya Geita kata ya Lwamgasa katika Kijiji cha Imalanguzu, mara baada ya kuwasili Naibu Waziri wa Madini Stanslausi Nyongo mgodini hapo akiwa na viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Madini, uongozi wa mkoa na viongozi wa dini kwa ajili ya kwenda kusitisha shughuli za uokoaji wa wachimbaji wadogo wawili Karos Msukuma Paulo mwenyeji wa Chato na Kulwa Joseph Mahungija mwenyeji wa Busolwa Nyang’wale waliofukiwa kifusi siku ya tarehe 1/10/2019.

Usitishaji wa zoezi hilo umefanyika tarehe 9/11/2019 ikiwa ni siku 39 tangu wachimbaji hao wafukiwe na kifusi kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika kipindi chote cha uokoaji. Ripoti maalam ya timu ya wataalam wa uokoji imeeleza kuwa kumekuwa na changamoto nyingi wakati wote wa ukoji zilizopelekea kuwa na ugumu wa kuwaokoa wachimbaji hao.

Akiwasilisha taarifa ya wataalam wa uokoaji iliyoishauri serikali kusitisha kwa zoezi hilo la uokoaji kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo,  mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga amemwambia Naibu Waziri wa Madini kuwa miongoni mwa changamoto zilizojitokeza wakati wa uokoaji ni pamoja na uwepo wa maji chini ya mgodi, mwingiano wa magogo mbalimbali chini ya shimo la mgodi, na kutokuwa na usalama katika eneo hilo hata kwa vyombo vya uokoaji.

Maganga aliongeza kuwa, kulikuwa na wataalam wa makundi mbalimbali ya uokoaji na vifaa vya kutosha kutoka kwa jeshi na uokoaji, mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), na makampuni mengine kutoka kwenye migodi mbalimbali, lakini pamoja na juhudi zote hizo imeshindikana kupatikana kwao.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa  siku ya tukio hilo, kwenye shimo hilo kulikuwa na wachimbaji 5 ambapo 3 kati yao waliokolewa siku hiyo hiyo na wawili hawakuweza kupatikana hadi zoezi hilo la uokoaji linasitishwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri Nyongo, akiongea kwa masikitiko na majozi kwenye hadhara hiyo, Nyongo amesema kwanza lililotokea ni bahati mbaya na kwamba serikali imesikitishwa na tukio hilo na kwamba iko pamoja wafiwa na wachimbaji wote.

Ameongeza kuwa, serikali inathamini sana hata uhai wa mtu mmoja kuliko dhahabu au madini yote yaliko chini na ndio maana inasisitiza wachimbaji kuchimba kwa kufuata utaratibu na sharia ili wachimbe kwa kuzingaatia usalama ili kuepukana na majanga kama hayo.

Nyongo ametowa kauli ya serikali ya kuhitimisha shughuli za uokoaji na kutoa maelekezo kuhusu eneo hilo ambalo wachimbaji hao wamefukiwa na kifusi.

“Na sasa tunakwenda kufanya ibada ya kwenda kuwazika wenzetu, viongi wetu wa dini wako hapa watatuongoza katika ibada hiyo kwa ajili ya maombi. Natamka kuwa, shughuli zote za uchimbaji katika eneo ambalo tunaamini kuwa ndipo wezentu hawa wapo, basi eneo hilo litambuliwe rasmi kuwa ndio kabuli lao na kama kuna undelezaji wa shughuli ya uchimbaji utaendelea katika eneo lingine na kwa utaratibu mwingine.” alisema Nyongo.

Nyongo pia alitoa maagizo kwa afisa madini mkazi mkoa wa Geita na timu yake kusimamia usitishwaji wa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo mpaka pale hatua za uzingatiaji usalama ziwe zimefuatwa ili kuepusha ajali nyingine.

Kwa upannde wake Mchungaji Nuhu Suleman alie ongoza ibada hiyo ya kuwaombea marehemu alisema, hapana budi kumshukuru mungu kwa kila jambo na kila jambo hukusudiwa na mungu. Amewakumbusha waumini wote kumuelekea mungu kwani yeye ndie mwenye upekee na ufalme na kwamba maisha ya binaadamu yana ukomo ni vyema kila mmoja akajiandaa na safari hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals