Tarehe : Feb. 12, 2024, 8:13 a.m.
● Ina uwezo wa kuchoronga miamba mpaka mita 400
●Lengo ni kuwa na mitambo 15 ifikapo Juni 2024
●Ulinganifu wa gharama za uchorongaji zinazotozwa ni asilimia 47.46 ambazo ni gharama za chini.
Na.Samwel Mtuwa - MoM
Mnamo Oktoba 21,2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alizindua mitambo mitano ya uchorongaji wa miamba aina ya Diamond Core Drilling (DD) ambayo ina uwezo wa kuchoronga miamba kwa mita 400 kuelekea chini ya ardhi.
Mitambo hiyo inayomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yenye lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kuweza kuchimba kwa uhakika bila kupoteza mitaji na muda.
Akizungumza katika semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyotolewa hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuwa na mitambo 15 ambayo itasambazwa katika sehemu za wachimbaji wadogo wa madini.
Aliyataja maeneo hayo ambayo ni Lwamgasa-Geita tayari mita 207 zimechorongwa, Itumbi- Chunya mita 150 Nyamongo -Tarime mita 153 , na Nhori - Dodoma mita 160 .
Akielezea kuhusu gharama za uchorongaji Dkt.Venance alifafanua kuwa gharama ya kuchoronga mita moja ni shilingi 227,587.50 ambayo sawa na dola 89.25.
Naye, Meneja wa uchimbaji mdogo kutoka STAMICO Tuna Bandom alifafanua kuwa kuhusu ulinganifu wa gharama za uchorongaji zinazotumika kwa mitambo ya wachimbaji wadogo kwa shimo moja lenye urefu wa mita mia (100m) unagharimu kiasi cha shilingi 108,012.52 ambazo ni sawa na dola za Marekani 42.36.
Bandoma aliongeza kuwa pamoja na gharama ndogo za uchorongaji zinazotozwa kwa wachimbaji wadogo pia wanapata huduma ya bure ya ushauri elekezi kutoka kwa wataalam wa jiolojia kuhusiana miamba inayochorongwa.
#Vision2030:MadiniNiMaishaNaUtajiri
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.