[Latest Updates]: Mahimbali Apokea Taarifa Maandalizi Wiki ya Madini Kutoka FEMATA

Tarehe : May 7, 2024, 7:56 a.m.
left

Maonesho na Kongamano la Wachimbaji Madini kufanyika Dodoma Juni 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amekutana na kuzungumza katika kikao kifupi na Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Madini, Maonesho na Kongamano la Wachimbaji Madini Tanzania.

Kikao hicho kimefanyika leo Mei 7, 2024 ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo Kamati hiyo imefika ofisini hapo ili kutoa taarifa ya maandalizi ya shughuli hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Mahimbali ameipokea taarifa ya maandalizi ya shughuli hiyo na kuwapongeza wajumbe wa Kamati hiyo kwa maandalizi ya shughuli hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) kwa kushirikiana na Wizara ya Madini.

Aidha, Wiki ya Madini, Maonesho na Kongamano la Wachimbaji Madini Tanzania linatarajiwa kufanyika June 20 mpaka 27, 2024 Jijini Dodoma ambapo Wachimbaji Wadogo, wa Kati, Wakubwa na Wadau wote wa Sekta ya Madini watashiriki.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Peter Kabepela amesema lengo la Wiki ya Madini, Maonesho na Kongamano la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania ni kutoa Dira ya FEMATA katika Mwaka wa Fedha 2024/25 kwa wadau mbalimbali wa Sekta hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals