[Latest Updates]: Maafisa Habari Nchini Washuhudia Mageuzi Mgodi wa Kiwira

Tarehe : Feb. 20, 2025, 5:56 p.m.
left

Watembelea Kiwanda cha kuzalisha  Mkaa wa Rafiki Briquettes
Mkaa wa Kiwira watajwa kuwa bora

Songwe

Maafisa Habari kutoka Wizara, Taasisi, Halmashauri na Wakala mbalimbali za Serikali  Februari 19, 2024 walitembelea  Mgodi wa Kiwira, Mkoani Songwe  kama sehemu ya mafunzo ya kutoa elimu kwa umma.

Ziara hiyo  ilikuwa  sehemu ya juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati safi, ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuongeza matumizi ya nishati safi kwa maendeleo endelevu.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba Chacha alisema kuwa Serikali inatoa msukumo mkubwa kwa wananchi na viwanda kutumia nishati safi, huku akiutaja mgodi wa Kiwira kama mfano wa mafanikio katika uendelezaji wa nishati safi. 

“Mhe Rais anazungumzia matumizi ya nishati safi, na tayari kama nchi tumefufua kiwanda chetu cha Kiwira, ambacho sasa kinasimamiwa na watanzania wenzetu, lengo ni kuhakikisha soko la ndani linaimarika na wanakuwa na mkaa wa kutosha,” alisema Dkt. Rioba.

Vilevile, alisisitiza kuwa mkaa unaozalishwa na Kiwira ni bora zaidi ukilinganisha na mkaa mwingine, na kuonyesha kuwa ni hatua nzuri katika kuboresha mazingira na kudhibiti matumizi ya kuni.

Kwa upande wake, Mhandisi Peter Maha
Mratibu wa Mradi wa Makaa ya Mawe Kiwira -Kabulo amesema Kuwa Mgodi huo ulianza rasmi mwaka 1980 kwa ajili ya uchimbaji wa makaa ya mawe kwa uzalishaji wa umeme na matumizi ya viwandani.

Alisema awali, Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ulinzi wa miundombinu, lakini hivi sasa, kiwanda hicho kimefufuka na kimekuwa sehemu ya dhamira ya Serikali ya kuendeleza matumizi ya nishati safi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, washiriki wa ziara hiyo walieleza kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi, hususan kwa kutumia mkaa wa Kiwira kwa ajili ya kupikia kwa kutumia makaa ya mawe hivyo, kusaidia kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa katika maandalizi ya chakula.

 Walisisitiza kuwa ni muhimu kwa jamii kuendelea kujifunza na kutekeleza mbinu bora za utunzaji wa mazingira ili kuendeleza ustawi wa taifa.

Wakiwa katika mgodi huo, maafisa hao walijionea mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika kiwanda cha Kiwira, ambacho kilikumbwa na changamoto nyingi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1980.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals