[Latest Updates]: Sekta ya Madini kuzalisha mamilionea – Waziri Biteko

Tarehe : March 12, 2020, 9:50 a.m.
left

Na Greyson Mwase, Dodoma

Waziri wa Madini Doto  Biteko amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini  kwa kushirikiana na Tume ya Madini inaendelea kuhakikisha inawawezesha wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ili waweze kuwa mamilionea huku Serikali ikipata mapato yake kutokana na kodi mbalimbali na kuinua Sekta ya Madini.

Waziri Biteko aliyasema hayo leo tarehe 12 Machi, 2020 kwenye ziara ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika katika machimbo ya mawe ya nakshi Ntyuka, Soko la Madini Dodoma na Chuo cha Madini Dodoma (MRI) yenye lengo la kufahamu utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

Katika ziara hiyo, Waziri Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

Alisema kuwa, ili kuhakikisha wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini wanaendesha shughuli zao kwa faida, Serikali imeweka mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini nchini na kupunguza kodi mbalimbali.

Akielezea  mikakati ya kuboresha masoko ya madini nchini yaliyoanzishwa tangu mapema Machi mwaka jana Waziri Biteko alieleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini inaendelea kuboresha miundombinu katika masoko husika ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mashine za kupima madini, mizani na kusomesha wataalam katika fani ya upimaji wa madini.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko alipongeza mgodi wa kuchimba mawe wa Ntyuka uliopo jijini Dodoma kwa kukiwezesha kikundi cha wakinamama 120 kwa kuwapatia mabaki ya mawe ambayo huyatumia kuzalisha kokoto ambazo huziuza na kujipatia kipato.

Wakati huohuo akizungumza kwa niaba ya kikundi cha wakinamama wanaozalisha kokoto katika eneo la Ntyuka jijini Dodoma Blandina Daudi mbali na kushukuru mgodi kwa kuwapatia mabaki ya mawe kwa ajili ya kuzalisha kokoto alieleza kuwa kupitia kazi  husika wameweza kufanya maendeleo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba na kusomesha watoto.

Awali akizungumza katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati ya Madini katika Soko la Madini la Dodoma, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Laurent Bujashi alisema kuwa kabla ya kuanzishwa kwa soko husika kwa kipindi cha miezi sita kabla, ukusanyaji wa mapato ulikuwa ni jumla ya shilingi milioni 118.4 ikiwa ni wastani wa shilingi milioni 23.6 kwa mwezi.

Bujashi aliendelea kueleza kuwa mara baada ya kuanzishwa kwa soko la madini Mei 19, 2019 makusanyo yaliongezeka hadi kufika jumla ya shilingi milioni 486.8 kwa kipindi cha miezi sita ikiwa ni wastani wa shilingi milioni 54.1 kwa mwezi na kusisitiza kuwa ongezeko hilo lilitokana na uwepo wa soko na uwazi katika biashara ya madini hususan dhahabu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals