[Latest Updates]: Tanzania Ina Akiba ya Karati Milioni 37.46 za Madini ya Almasi

Tarehe : Feb. 18, 2024, 10:09 p.m.
left

●Mgodi uligundulika mwaka 1940.

●Mpaka sasa mgodi una miaka 84 ya uchimbaji.

●Serikali inamiliki asilimia 25 ya hisa.

● Mgodi unaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 50 mbele.

Na.Samwel Mtuwa - Shinyanga

Tafiti zinaonesha kuwa kuna kiasi cha akiba ya karati milioni 37.46 za madini ya Almas katika mgodi wa almas wa Mwadui uliopo mkoani Shinyanga katika Wilaya ya Kishapu.

Hayo yamebainishwa leo Februari 18, 2024 na Kaimu Meneja wa Mgodi wa Almas Mhandisi Shaghembe Mipawa wakati akiwasilisha mada katika semina  kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini.

Mhandisi Mipawa ameongeza kuwa kisheria ukomo wa leseni  utakuwa mwaka 2033 ambapo   leseni itakuwa imemaliza muda wake lakini tafiti zinaonesha  rasilimali ya madini ya almas yaliyopo katika mgodi  yanaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 50 mbele hii ni kutokana makadilio ya rasilimali iliyopo.

Akielezea kuhusu umiliki wa mgodi Mhandisi Mipawa ameeleza kuwa kwasasa Serikali inaumiliki wa hisa kwa asilimia 25 na kampuni ya Petra Diamonds inaumiliki wa hisa kwa asilimia 75 ambapo mchango wa mgodi kwa jamii (CSR) ni asilimia 0.7 kwa mujibu wa sheria.

Naye , Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa akifafanua kuhusiana na mchakato wa kuongeza hisa za  umiliki kwa Serikali amesema kuwa Serikali na taasisi wadau ipo katika majadiliano juu ya kuongeza hisa kufikia asilimia 37 kwa Serikali na asilimia  63 kwa kampuni ya Petra Diamond.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe.Kilumbe Ng'enda ameupongeza mgodi kwa kazi nzuri inayofanya ikiwa pamoja na kuitikia maelekezo yanayotolewa na Kamati katika kutekeleza majukumu yao.

Akitolea mfano juu ya Ujenzi wa Bwawa jipya  la maji taka (TSF) unaoendelea katika mgodi,  kuwa hii ni ishara tosha kuwa mnasikiliza maelekezo kutoka kwa wajumbe wa kamati na kuyafanyia kazi ni imani yetu kuwa mtaendelea na utekelezaji wa maagizo mengine kama yatakavyotolewa kwenu.

Mgodi wa Almasi wa Mwadui uligundulika mwaka 1940 , una hekali za mraba 146 ukiwa ni moja ya mgodi mkubwa wa mwamba wa Kimberite duniani ambapo uchimbaji wake unafanyika kwa njia ya wazi yaani Open Pit.

#VISION2030:MadiniNiMaoshaNaUtajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals