[Latest Updates]: Dondoo Aliyoyasema Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa Katika Kipindi cha Jambo Tanzania Tarehe 13 Novemba, 2024

Tarehe : Nov. 13, 2024, 4:21 p.m.
left

Kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2024

DONDOO ALIYOYASEMA NAIBU WAZIRI WA MADINI, DKT. STEVEN KIRUSWA KATIKA KIPINDI CHA JAMBO TANZANIA TAREHE 13 NOVEMBA, 2024

Royal Tour imeleta wawekezaji
Royal tour imeongeza mwamko wa wawekezaji kuja kuwekeza kwenye Sekta ya Madini Tanzania. Madini tunayo na wawekezaji wameendelea kuja. Kuna ongezeko la wazalishaji, Wadogo, wa Kati na Wakubwa.

Ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Madini ya Metali
Mwekezaji wa sasa Kampuni ya Tembo Nickel Refining Limited itakayojenga kiwanda cha kusafisha madini ya metali hivi sasa yupo kwenye mchakato wa kujenga Kiwanda cha kisasa cha kusafisha madini hayo, katika eneo la Mgodi wa unaofungwa wa Buzwagi pale Kahama mkoani Shinyanga. 

Mkakati wa Tanzania kuongeza thamani Nchini
Mkakati wa kuyaongezea thamani madini hapa nchini upo bayana. Tunataka kama taifa kuhakikisha taifa linajengewa uwezo wa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya kuchakata madini mkakati  hapa hapa nchini hatua hii itasaidia kulinda ajira za watanzania.

Minada ya Madini ya ndani na nje ya Nchi Mbioni
Katika mwelekeo wa kuendelea kutangaza madini yetu na kuongeza masoko tutaanzisha minada ya madini ya vito ya ndani na ya kimataifa, minada ya ndani inatarajiwa kufanyika katika miji ya Arusha, Dar Es Salaam na Zanzibar.

Utoroshaji Madini
Kukosekana kwa masoko ya madini kulichangia utoroshaji wa madini kwasababu hakukuwa na mfumo rasmi lakini pia baadhi walikosa uzalendo. Tunaendelea kuzunguka nchi nzima kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kutumia masoko. Kwa kushirikiana na Vyombo vya dola tumeendelea kudhibiti utotoshaji wa madini hadi katika viwanja vya ndege. Tumeanzisha masoko 43 na vituo vya ununuzi 105 kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji wa madini na hatimaye kulinda mapato ya Serikali.

Mazingira Wezeshi shughuli za Madini
Serikali imeendelea kupeleka huduma mbalimbali kwenye shughuli za madini ikiwemo miundombinu ya barabara, umeme kuhakikisha shughuli za madini zinafanyika vizuri kuongeza tija.


Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR)
Tumeweka Sheria na Kanuni zinzomtakamwekezaji kuwajibika kwa jamii inayomzunguka Ili wanufaike na uwekezaji wao. Kwanza hapatuna dhana mbili, moja kuwajibikakwa jamii, pili inamtaka atoe ajira kwa watanzania wanaozunguka maeneo ya uwekezaji kupitia utoaji huduma migodini.

Maudhui ya Ndani (Local Content)
Tumefanikiwa kutengeneza Sheria na Kanuni zinazowataka wamiliki wa migodi kununua bidhaa na huduma ambazo zinapatikana hapa nchini basi wanunulie hapa na kutoka kwa watanzania, kufanya hivyo kutoka kwa Kampuni za Watanzania, na tangu ianze kutekelezwa imeleta mabadiliko makubwa sana katika sekta ya madini na wananchi waliopo katika maeneo shughuli za madini zinapofanyika ni mashahidi katika hili.

Mazingira
Kabla ya mwekezaji kufanya shughuli za uchimbaji ni lazima aandae taarifa ya athari za mazingira namna ya kurejesha katika hali yake ya asili baada ya uchimbaji. Madini kama Uranium tathmini yake inafanyika kwa mapana zaidi, Sisi wizarani tuna vitengo vyote vinavyosimamia masuala ya afya, usalama na utunzaji mazingira kikiwemo cha ukaguzi wa migodi.

Matumizi wa Zebaki
Tanzania inachukua hatua kila siku kwa kuhamasisha matumizi yateknolojia rahisi na kuachana na matumizi ya zebaki tunapoelekea katika kipindi cha ukomo wa matumizi haya.

Tuna Jambo Letu Dar Es Salaam Novemba 19- 21, 2024
Kila mwaka tunakutana katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini, Ni mkutano unaotumika kutangaza fursa zetu za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ikihusisha watoa mada kutoka ndani na nje. Ninawahamasisha wadau mbalimbali kujisajili ili kushiriki Mkutano huo muhimu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals