[Latest Updates]: Waziri Gwajima Azindua Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Mwaka 2023

Tarehe : March 8, 2024, 1:06 p.m.
left

Wanawake Madini wajivunia mchango wao Sekta ya Madini

Waungana na wenzao kusherekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Mwaka 2023 itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuleta usawa wa kijinsia katika nyanja zote nchini.

Ameyasema hayo wakati akizindua Sera hiyo leo Machi 8 2024 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani katika Viwanja vya Mashujaa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo alimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa. 

Dkt. Gwajima amesema kuwa halikuwa jambo dogo ila limewezakana kwa ushirikiano wa wadau wote kisekta, umma na binafsi na wananchi kwa ujumla na kwamba hatua hiyo ni juhudi za Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuunda Wizara ya Jamii na kupelekea kupiga hatua nyingine katika historia ya nchi Tanzania.

Wakati huohuo, Watumishi Wanawake wa Wizara ya Madini wameungana na wenzao duniani kote kusherekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8.

Akizungumzia Maadhimisho hayo, Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Wizara ya Madini kupitia TUGHE,  Veneranda Charles amesema kuwa Watumishi Wanawake wa Wizara wanajivunia kwa kuwa sehemu ya mageuzi makubwa katika Sekta ya Madini.

Amesema kuwa, katika miaka ya karibu idadi ya Wanawake katika Sekta ya Madini imeongezeka kwa kiasi kikubwa wakihudumu kama wataalam katika nafasi tofauti ikiwemo ya Jiolojia, Uchenjuaji na Uhandisi wa Migodi ambazo miaka ya nyuma mwitikio haukuwa mkubwa sana kwa Wanawake tofauti na hivi sasa.

Veneranda ameongeza kuwa hatua hiyo inatotokana na mazingira wezeshi yaliyowekwa na Serikali kupitia Wizara kwa Wanawake kufanya kazi na kuchangia katika maendeleo ya Sekta na taifa kwa ujumla.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 ni Wekeza kwa Wanawake: Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii

VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals