Tarehe : Aug. 15, 2024, 6:04 p.m.
DODOMA
Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Wizara ya Mipango na Uwekezaji pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara zimekutana kujadili namna ya kuondoa changamoto katika sekta ndogo ya chumvi nchini.
Wizara hizo zimekutana leo Agosti 15 , 2024 jijini Dodoma kufuatia taarifa zilizowasilishwa kwa Serikali na Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA) kuhusu changamoto zinazoikabili sekta hiyo ndogo ya chumvi ikiwemo kudorora kwa biashara ya chumvi hapa nchini.
Kikao hicho kilijumuisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Jaffo ,Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mh. Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde pamoja na Wadau wa Chumvi Nchini.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa,Wizara ya Madini kupitia STAMICO imewahakikishia wadau juu ya ufungwaji wa kiwanda cha kusindika Chumvi katika Wilaya ya Kilwa,Mkoa wa Lindi kabla ya
Mwisho wa Mwezi Desemba 2024.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.