[Latest Updates]: Wachimbaji Wadogo Kuendana na Tecknolojia ya Kisasa

Tarehe : Oct. 21, 2023, 4:30 p.m.
left

Mitambo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.2 yazinduliwa

Serikali yapanga kufanya Utafiti nchi nzima

Yasaini Hati ya Makubaliano na Mikataba

Katika mikakati ya kuendeleza wachimbaji wadogo wa madini nchini Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imezindua mitambo mitano ya kisasa ya uchorongaji miamba yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.2 lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuchimba madini bila kubahatisha.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 21, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa mitambo mitano ya uchorongaji miamba na kushuhudia STAMICO ikisaini hati ya makubaliano Kampuni ya FLUXING Ltd na pamoja na hati ya makubaliano kati ya STAMICO na Chama Kikuu cha  Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Tabora (WETCO) jijini Dodoma.

Rais Dkt .Samia amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo wa madini katika Pato la Taifa ambapo mpaka sasa inachangia asilimia 40.

Akielezea kuhusu mikakati iliyopo Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa Serikali kupitia STAMICO  itawajengea uwezo wazalishaji wa chumvi mkoani Mtwara na Lindi  kwa kujenga kiwanda kikubwa cha usafishaji wa chumvi ili ipate ubora unaostahiki na kutoa shamba darasa kwa wazalishaji wa chumvi.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameishukuru Serikali na ameiomba iendelee kuunga mkono Vision 2030 katika kufanya utafiti wa kina wa jiofizikia nchi nzima lengo ni kupata taarifa za miamba ili kuwa na kanzidata yenye taarifa zote.

Akielezea kuhusu Madini Mkakati Mhe.Mavunde amefafanua kuwa hivi sasa mahitaji ya Madini Mkakati ni tani milioni kumi , ifikapo mwaka 2050 mahitaji ya madini mkakati yataongezeka na kufikia tani milioni 150, hivyo Serikali kupitia Wizara ya Madini inatakiwa kuweka mikakati ya kuingia katika uchumi mkubwa wa dunia kupitia madini ya kimkakati.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwase  amesema kuwa STAMICO inaendelea kushirikiana na vyama vya wachimbaji wadogo ili kuendelea kuwajengea uwezo kwa kuwapatia  vifaa na ushauri wa kitaalam katika maeneo yenye changamoto za tafiti, uchimbaji na uchenjuaji.

Aidha, Mwenyekiti wa Umoja  wa Mabenki Tanzania (TBA) Theobas Sabi ameipongeza STAMICO kwa juhudi mbalimbali inazofanya katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwajengea imani baina ya wachimbaji na Taasisi za fedha katika utoaji wa mikopo.

Sabi ameongeza kuwa, changamoto kubwa kwa wachimbaji wadogo ni kukosekana kwa taarifa za uhakika wa mashapo katika maeneo yao ya uchimbaji, hivyo ameshauri  kuendelea kufanya tafiti ili taarifa zitakazopatikana zitumike kama dhamana ya mikopo kwa wachimbaji.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals