[Latest Updates]: STAMICO Yaieleza Kamati ya Bunge Nishati na Madini Mpango wa Uwekezaji

Tarehe : June 11, 2024, 10:40 p.m.
left

●Katibu Mkuu aieleza Kamati Mipango kabambe kuiendeleza STAMICO , STAMIGOLD

Dodoma

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupitia kampuni tanzu ya STAMIGOLD leo Juni 11, 2024 limewasilisha mpango wa uwekezaji wa kampuni ya STAMIGOLD kuhusu uendelezaji wa miradi ya madini kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Deusdedith Magala amesema kuwa tangu kuanza uzalishaji hadi kufikia Machi, 2024 mgodi umezalisha na kuuza jumla ya wakia 122,964.53 za madini ya dhahabu na wakia 16,662.54 ya madini ya fedha.

Magala ameeleza kuwa mgodi umeendelea na uhakiki na utafiti kupitia njia mbalimbali za ukusanyaji wa taarifa na ukadiriaji  upya wa akiba ya mashapo ya mgodi ambapo mpaka April, 2024 mgodi ulikuwa na akiba ya mashapo ya wakia za dhahabu 114,190 ambazo zitachimbwa kwa miaka mitano.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Nishati na Madini, Mathayo David Mathayo ameitaka wizara  kuisimamia na kufuatilia kwa karibu  kampuni  ya STAMIGOLD  ili iwe kampuni yenye manufaa.

Akizungumza kuhusu  wajibu wa mgodi kwa jamii (CSR),Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amesema kuwa wizara imepokea maoni yaliyowasilishwa na kamati kuhusu mapitio ya kanuni za CSR na kuzifanyia kazi ya kuziboresha itakapobidi.

Naye , Katibu Mkuu Wizara ya Madini,Kheri Mahimbali amesema Malengo ya Wizara ni kuipeleka mbali  Stamigold ili uwe mgodi mkubwa utakao tambaa sehemu mbalimbali ndani ya nchi pamoja na kutambulika na taasisi kubwa za fedha.

STAMICO ilianzishwa rasmi mwaka 1972 kwa lengo la kuwekeza kimkakati katika miradi ya madini na uvunaji wa  rasilimali madini ndani ya  mnyororo mzima wa sekta ya madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals