[Latest Updates]: Profesa Msanjila Afungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji Geita

Tarehe : Sept. 23, 2020, 11:10 a.m.
left

Leo tarehe 23 Septemba, 2020 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amefungua kongamano la biashara na uwekezaji katika Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji wa Bomba Mbili Mjini Geita.

Kongamano hilo lilikutanisha wadau wa madini kwa lengo la kujadili na kujenga uelewa wa pamoja wa fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini ndani ya mkoa wa Geita.

Wadau walioshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na wawakilishi kutoka  Wizara ya Madini na Taasisi zake, Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Kampuni za Uchimbaji wa Madini, Wawakilishi kutoka Chama cha Wachimbaji wa Madini wa Mkoa wa Geita (GEREMA) Benki Mbalimbali na Taasisi nyingine za Serikali.

Kupitia hotuba yake Profesa Msanjila aliwataka wananchi wa mkoa wa Geita kuchangamkia fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwenye kampuni zinazojihusisha na uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na ulinzi, vyakula n.k.

Akielezea mafanikio katika Wizara ya Madini, Profesa Msanjila alieleza kuwa ni pamoja na ukusanyaji wa maduhuli kutoka shilingi bilioni 160 hadi  shilingi bilioni 528 ndani ya kipindi cha miaka mitano, ongezeko la  kasi ya utoaji wa leseni za madini, kutengwa maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini.

Katika hatua nyingine Profesa Msanjila aliziomba  taasisi za kifedha kutokusita kutoa mikopo  kwa wachimbaji wa madini na wajasiriamali wanaotoa huduma kwenye kampuni za uchimbaji wa madini.

Aidha, Profesa Msanjila aliwataka wananchi kuzalisha bidhaa bora ili kupata soko la uhakika kwenye kampuni zinazochimba madini.

“Nia yetu kama Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Madini inawezesha ukuaji wa sekta nyingine kama vile kilimo na uvuvi, tunatamani kuona hata madini yakiisha, kunakuwepo na ukuaji wa sekta nyingine zitakazowezesha uchumi wa nchi kupaa.

Aidha, Profesa Msanjila aliipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Wizara ya Madini na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya maonesho hayo.

Taasisi zilizopo chini ya Wizara zinazoshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Mgodi wa STAMIGOLD.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals