[Latest Updates]: Naibu Waziri Nyongo atembelea ofisi ya Madini Kigoma

Tarehe : Nov. 1, 2018, 5:09 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ametembelea Ofisi ya Madini Kigoma na kuzungumza na wafanyakazi, akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Machi 3 mwaka huu.

Mjiolojia katika Ofisi ya Madini Kigoma, Laurent Bujashi (kushoto) akimwonesha Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) aina za Madini yanayopatikana mkoani humo, wakati Naibu Waziri alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na wafanyakazi, akiwa katika ziara ya kazi Machi 3 Mwaka huu.[/caption]

Katika kikao hicho, wafanyakazi walipata fursa ya kujadiliana na Naibu Waziri kuhusu utendaji kazi katika eneo lao, yakiwemo mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo.

Naibu Waziri aliwapongeza wafanyakazi hao kwa utendaji kazi mzuri na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto walizowasilisha, ikiwemo upungufu wa watumishi.

Hata hivyo, aliwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuhakikisha wanakusanya maduhuli ya Serikali kwa kiwango kinachotakiwa ili Sekta hiyo iweze kukuza mchango wake katika Pato la Taifa.

Imeandaliwa na:

Veronica Simba, Kigoma

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

Kikuyu Avenue,

P.O Box 422,

40474 Dodoma,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

BaruaPepe: info@madini.go.tz,                                             

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals