[Latest Updates]: Waziri Mavunde Atatua Mgogoro wa Mipaka ya Leseni Mirerani

Tarehe : Jan. 16, 2025, 1:35 p.m.
left

Awataka wachimbaji wote nchini kuzingatia sheria na kanuni za madini

Alekeza Maafisa Madini kusimamia sheria ili kupunguza migogoro kwenye sekta ya Madini

Dodoma

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amewataka wachimbaji kote nchini kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima.

Mh Mavunde ameyasema hayo jana Jijiji Dodoma wakati wa kikao cha kutatua mgogoro wa mipaka ya Leseni uliyopo kati ya Kampuni ya Njake na Ndg. Patrick Miroshi, ambapo alizikutanisha pande zote mbili zenye mgogoro huo na kujadili kwa pamoja namna ya kutatua mgogoro huo na mwishoni kufikia muafaka wa kila mmoja kuendelea na uchimbaji katika eneo la leseni yake kwa amani.

“ Serikali inatamani kuona Sekta ya Madini inaendelea kukua na kutoa mchango wa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu,migogoro siku zote inaturudisha nyuma katika jitihada za kuongeza uzalishaji na kuchochea Uchumi.

Ni maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa haraka wa migogoro kwenye sekta ya madini ili kuchochea ukuaji wake.

Niwatake maafisa Madini wote nchini kusimamia sheria na kanuni ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima na pia niwatake wachimbaji wote kuzingatia sheria katika shughuli zao za kila siku”, alisema Mavunde. 

Baada ya Taarifa ya Timu ya wataalamu iliyoundwa na Waziri Mavunde ilielekezwa nankuridhiwa kuwa Pande mbili hizo kila mmoja kurejea kwenye eneo la mipaka ya Leseni yake na Kampuni ya Njake kumfidia Ndg. Miroshi gharama alizoingia awali za uchimbaji.

Kikao hicho cha usuluhishi kilihudhuriwa na viongozi wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Mhandisi Yahya Samamba na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals