[Latest Updates]: Aliyoyasema Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati Akizungumza na Watumishi wa Wizara na Taasisi zake mara baada ya Kuwasili Wizarani tarehe 10 Januari, 2022

Tarehe : Jan. 10, 2022, 3:12 p.m.
left

Kwanza namshukuru Mungu kwa kuifanya tarehe ya leo kuwa tofauti kwani tunapokea viongozi wapya. Pili Mhe. Rais kutuongezea nguvu kwa mara moja na kutufanya tutanuke.

Nawapongeza ninyi kwa kuja wizara ya madini, ni Wizara ndogo lakini ina matarajio makubwa kwa nchi yetu na wananchi. Ujio wenu unakuja si tu kutuchangamsha bali mtakuja na mawazo mapya na vingine mlivyokuwa mnaviona nje vitasukuma Sekta mbele.

Nina furaha kubwa kwasababu wote walioteuliwa nina wafahamu. Naibu Waziri tulikuwa naye Bungeni ni Daktari Mbobezi, Katibu Mkuu namfahamu umefanya naye kazi akiwa kwenye Kamati ya Majadiliano ya Serikali anauelewa mpana kwenye Sekta na ninaamini Naibu Katibu Mkuu atakuja na ubunifu wa kukusanya zaidi na kuifanya wizara kuwa imara.

Ninawashukuru Katibu Mkuu anayeondoka Prof. Simon Msanjila na Naibu Waziri Prof. Shukrani Manya kwa namna walivyonisaidia. Prof. Msanjila nimefanya naye kazi muda mrefu na tulishirikiana sana. Hapakuwa na jambo lolote ambalo Katibu Mkuu alifanya bila kunishirikisha au mimi kumshirikisha. Alikuwa msaada wa kufanya timu hii iende mbele. Tunatarajia muwe karibu na sisi. Naibu Katibu Mkuu unaingia kwenye rekodi ya kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Kwanza Wizara ya Madini.
 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals