[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yasaini Mkataba Ujenzi wa Jengo la Ghorofa Nane la TGC

Tarehe : June 26, 2024, 11:06 p.m.
left

WIZARA YA MADINI YASAINI MKATABA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 8 LA TGC

-Kampuni za wazawa zaungana kulijenga

-Lengo kuifanya Tanzania kuwa Kitovu cha Madini ya Vito Afrika

Wizara ya Madini imesaini Mkataba wa Ujenzi wa Jengo la kisasa la ghorofa nane la Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC) na Kampuni mbili za wazawa zilizoungana za Skywards na Lumocons. 

Hafla hiyo imefanyika leo Juni 26, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Prof. AbdulKarim Mruma jijini Dodoma na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa.

 Kwa upande wa Wizara, Mkataba ho umesainiwa na Katibu Mkuu Kheri Mahimbali huku Mkurugenzi wa Kampuni Lumocons Limited Innocent Shirima akisaini kwa niaba ya Kampuni hizo mbili za ujenzi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Kiruswa amewataka wazabuni hao kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa ubora na muda unaotakiwa na kwamba Wizara ya Madini itatoa ushirikiano ili kuhakikisha kutokuwepo kwa vikwazo vyovyote muda wote wa ujenzi.

“Niwapongeze kwa kushinda zabuni hii, lakini niwaeleze kuwa ujenzi wa mradi huu utawafikisha mbali na kuwatangaza kama mtatimiza yote yaliyopo kwenye mkataba huu" amesema Dkt. Kiruswa. 

Aidha, ameelezea umuhimu wa jengo hilo kwa kusema kuwa miundombinu iliyopo sasa haikidhi mahitaji ya Kituo hicho ambacho pia kina chuo cha kuongezea thamani madini ya vito, hivyo kukamilika kwa mradi huo utasadia sana katika utekelezaji wa shughuli za kituo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amesema kuwa lengo la Wizara ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha madini ya vito barani Afrika na kwamba Serikali iko mbioni kurejesha Minada ya Madini ya Vito na bidhaa za vito, hivyo kukamilika kwa mradi huo utasadia katika Uongezaji Thamani Madini hayo hapa nchini kwa wingi na kwa ubora vya kimataifa.

Naye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lumocons ameishukuru Wizara ya Madini kwa kuwaamini na kutoa zabuni hiyo na kusema kuwa watatekeleza ujenzi wa mradi huo kwa ubora, kiwango na wakati kwa mujibu wa mkataba, huku akisema ni fursa kubwa kwao kama Kampuni za wazawa.

Ujenzi wa Jengo hilo la TGC utagharimu kasi cha shilingi bilioni 33.42 (33,429,365,267.00) mpaka kukamilika.

TGC ni kituo kinachojihusisha na kutoa elimu, mafunzo, na huduma mbalimbali zinazohusiana na madini na vito vya thamani. Majukumu yake ni pamoja na kutoa mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito ikiwemo kukata, kung'arisha na huduma za kitaalam kwa wafanyabiashara na watengenezaji wa vito kuhusu uongezaji thamani madini hayo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals