[Latest Updates]: Shanta Mining yatakiwa kukamilisha ulipaji fidia

Tarehe : July 28, 2017, 9:08 a.m.
left

Serikali imeiagiza Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Shanta Mining Limited inayofanya shughuli zake Mkoani Singida kuharakisha ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao ili shughuli za uchimbaji zianze mara moja.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).[/caption]

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alitoa agizo hilo Desemba 12, 2017 wakati wa ziara yake ya kutembelea migodi ya dhahabu katika wilaya za Ikungi na Manyoni ili kujionea shughuli zinazoendelea pamoja na kuzungumza na wachimbaji wa madini.

“Mchakato wa fidia ufanyike haraka na mgodi uanze shughuli zake za uchimbaji mapema,” aliagiza Naibu Waziri Nyongo.

Akiwa njiani kuelekea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Elizabeth Shango uliopo katika Kijiji cha Sambaru, msafara wake ulisimamishwa na wananchi katika Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi ambao walilalamika kuzuiwa kuendeleza maeneo yao na kampuni hiyo na huku wakicheleweshewa kulipwa fidia.

Walisema kuwa tayari wameachia maeneo waliyokuwa wakimiliki kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo na uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu ili kupisha shughuli za uchimbaji mkubwa lakini Kampuni hiyo ya Shanta bado haijakamilisha ulipaji wa fidia.

Wananchi hao vilevile walimuomba Naibu Waziri Nyongo kuiagiza kampuni hiyo kuwapatia maeneo yaliyo wazi ili wafanye shughuli za uchimbaji.

Kufuatia malalamiko hayo, Naibu Waziri Nyongo aliiagiza kampuni hiyo kuhakikisha inakamilisha taratibu za ulipaji wa fidia bila kuchelewa ili shughuli za uchimbaji zianze mapema iwezekanavyo.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya Shanta Mining Limited (hawapo pichani) alipotembelea eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo.[/caption]

“Wananchi wanayo hoja ya msingi na inapasa wasikilizwe, ili taratibu zifanyike bila kuwepo migongano isiyokuwa ya lazima,” alisema.

Aliiagiza kampuni hiyo kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo pamoja na Uongozi wa Vijiji kujenga mahusiano bora baina yao na wananchi.

Nyongo alisema ili kupunguza migogoro baina ya kampuni na wananchi ni busara wakapatiwa maeneo ili wafanye shughuli za uchimbaji.

“Wapeni na wao maeneo wachimbe, busara itumike kuwapatia maeneo mazuri ili kujenga mahusiano mazuri,” aliagiza Naibu Waziri Nyongo.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo, Mhandisi Philbert Rweyamamu alisema kuchelewa kwa mchakato wa ulipaji fidia kumetokana na migongano ya kijamii.

Alisema kutokana na wananchi kutokuwa na elimu sahihi ya faida ya mradi wamekuwa wakileta vikwazo katika hatua mbalimbali za mchakato wa fidia.

Imeandaliwa na:

Mohamed Saif,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals