[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yababinisha Mikakati Yake kwa Wachimbaji Wadogo Dodoma

Tarehe : Oct. 15, 2024, 11:23 a.m.
left

●Mkakati wa kuwaendeleza na kuwasogezea huduma za Ugani mkoani Dodoma

●Mkakati wa kuwapatia maeneo mapya yaliyofanyiwa utafiti wa kina

●Mkakati wa kujenga Maabara mpya ya kisasa mkoani Dodoma

 Na.Samwel Mtuwa - Dodoma

Imeelezwa kwamba katika kuendeleza shughuli za uchimbaji mdogo wa madini nchini na kuhakikisha  rasilimali madini zinaongoza kuchangia katika Pato la Taifa , wizara na taasisi zake zinaendelea kutekeleza mikakati na mipango kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 15, 2024 na Waziri na Madini wakati akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalibali zilizoibuliwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

Akielezea kuhusu mikakati iliyopo ndani ya wizara kupitia bajeti ya mwaka 2024/2025, Waziri Mavunde amesema kuwa, katika kuimarisha uchimbaji wenye tija na uhakika serikali itajenga maabara ya kisasa mkoani Dodoma na Geita ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupeleka sampuli zao kwa uchunguzi.

Waziri Mavunde ameongeza kuwa , wizara itaendelea kutumia mpango wa ushirikiano baina ya taasisi za Umma na taasisi za sekta binafsi katika kuendeleza miundombinu ya barabara na nishati ya umeme sehemu zenye uchimbaji.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa madini Dkt. Steven Kiruswa  ameeleza kuwa, elimu kuhusu tozo zinazotozwa, wajibu wa mmiliki wa leseni kwa jamii , ushiriki wa watanzania katika uvunaji wa rasilimali madini na utunzaji mazingira katika shughuli za uchimbaji ilitolewa kwa wachimbaji wadogo katika Kamati za Maendeleo za Kata.

Awali , akiwalisha taarifa kuhusu mikakati ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo na kuwasogezea huduma za Ugani katika mkoa wa Dodoma kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini , Kamishna wa Madini Dkt. AbdulhRaman Mwanga amesema, wizara itaendelea kutoa elimu kuhusu matumizi salama ya zebaki katika wilaya ya Chamwino na Bahi.

Sambamba na hapo Dkt. Mwanga amesema , wizara itaendelea kuboresha mifumo ya utoaji na usimamizi wa leseni za madini pamoja na kuwezesha utafutaji wa madini kwa njia ya uchorongaji.

Mikakati mingine ni pamoja na kutoa elimu kuhusu athari za mazingira zitokanazo na uchimbaji wa madini ujenzi, elimu kuhusu tozo za madini na haki madini katika wilayani ya Dodoma na vitongoji vyake.

Aidha , Mwenyekiti wa Kamati wa Kamati ya Bunge Nishati na Madini Dkt.David Mathayo David, ameipongeza wizara kwa juhudi mbalimbali inazofanya katika mnyororo mzima wa thamani madini kutoka asilimia 7.1 mpaka kufikia asilimia  9 katika kuchangia Pato la Taifa.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, mkoa wa Dodoma una jumla ya watu 260,505 wanajihusisha na shughuli mbalimbali  kwenye mnyororo wa thamani wa uchimbaji mdogo ambapo kati ya hao wanaume ni 126,841 na wanawake ni 133,664 ambayo sawa na asilimia 4.6 ya watu wote wanaojishughulisha na shughuli hizo nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals