[Latest Updates]: Naibu Waziri Nyongo awaongoza Wabunge wa Afrika Kusini kujifunza usimamiaji wachimbaji wadogo

Tarehe : June 21, 2018, 4:19 a.m.
left

Ziara ya Kamati ya Jamii na Masuala ya Usalama ya Bunge la Jimbo la Ghanteng, Afrika Kusini, ambao wapo nchini kujifunza na kupata uzoefu namna Tanzania inavyoendesha sekta ya madini, imeendelea kwa wabunge hao kuwatembelea wachimbaji wadogo wa dhahabu waliopo eneo la Nori, wilayani Bahi.

Wakiongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Wabunge hao walifanya ziara hiyo Juni 20, 2018, ambapo walipata fursa ya kujionea shughuli za uchimbaji wa dhahabu unaofanywa na wachimbaji wadogo katika eneo hilo na kuzungumza nao kuhusu uzoefu wao katika kazi husika.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Kiongozi wa Ujumbe huo, S. Khanyile alikiri kuwa, ziara husika imewawezesha kujifunza mambo mengi na kwamba watatumia uzoefu walioupata kuboresha na kuimarisha zaidi sekta ya madini nchini kwao.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Nyongo aliwahakikishia Wabunge hao kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano kati yake na nchi ya Afrika Kusini, hususan katika sekta ya madini.

Alisema, ushirikiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya madini, utasaidia kuimarisha na kuboresha zaidi sekta husika na hivyo kuziwezesha kuwa za mfano katika uchangiaji wa Pato la Taifa na kuimarisha uchumi wa nchi na wananchi wake kwa ujumla.

Juni 19, mwaka huu, Wabunge hao walifika Makao Makuu ya Wizara ya Madini jijini Dodoma, ambapo walipokelewa na Waziri mwenye dhamana, Angellah Kairuki. Katika siku hiyo ya kwanza ya ziara yao, walipata fursa ya kujifunza kuhusu sekta husika kupitia uwasilishwaji wa Mada mbalimbali uliofanywa na Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa.

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Pichani ni matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals