Tarehe : Feb. 21, 2024, 11:59 a.m.
Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imetembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichopo jijini Mwanza leo tarehe 20 Februali,2024 na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi
Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Ndugu Deus Clement Sangu imeona maendeleo mazuri ya usafishaji wa dhahabu kiwandani hapo ikilinganishwa na kipindi cha nyuma walipotembelea kiwandani hapo
Aidha Mwenyekiti wa Kamati ameipongeza Serikali kupitia STAMICO kwa kuongeza mapato yake pamoja na kuanzisha kiwanda hicho ambacho kitapelekea STAMICO kupata mapato na nchi kupata faida mbalimbali kutokana na usafishaji wa dhahabu nchini
Katika wasilisho lake la kamati Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Dkt Venance Mwasse alielezea utekelezaji wa shughuli za kiwanda pamoja na changamoto ya kiwanda ya kutokupata dhahabu ghafi kwa wingi kutokana na maswala mbalimbali ikiwemo changamoto ya kikodi.
Kamati iliahidib kuifanyia kazi changamoto hii ya kikodi kwa kushirikiana na Serikali ili kiwanda kiweze kupata malighafi ya kutosha na kufanya kazi vizuri
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo aliishukuru kamati ya PIC kwa ushauri wao wanaoutoa mara kwa mara kwa Shirika kuhusu maswala ya uwekezaji nakupelekea Shirika kuendelea kufanya vizuri
Ziara hii ya Kamati itahusisha kutembelea miradi mingine ya Shirika ya STAMIGOLD na Makaa ya mawe Kiwira ili wajumbe wajionee uwekezaji wa STAMICO katika miradi mbalimbali.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.