[Latest Updates]: Mnada wa Madini ya Vito Kuzinduliwa Rasmi Tarehe 14 Desemba 2024 Mirerani, Manyara,

Tarehe : Dec. 12, 2024, 7:43 p.m.
left

▪Waziri Mavunde kuzindua Mnada Rasmi

▪Lengo ni kuyaongezea thamani
▪Kudhibiti utoroshaji
▪Kuuzwa kwa bei ya ushidani

MANYARA: WAZIRI wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mnada wa  madini ya  vito  unaotarajiwa kufanyika katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, ili kuyaongezea thamani madini hayo.

Mnada huo ambao ulisimama kwa muda, umepangwa kufanyika tena kwa mara ya kwanza Desemba 14, 2024.

Akizungumza leo Desemba 12, 2024, Mheshimiwa Mavunde amesema madini ya vito, yanafanyiwa mnada kama mkakati wa kuyatangaza na    kuyaongezea thamani kimataifa.


Mheshimiwa  Mavunde amesema utaratibu wa kufanya mnada huo ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

Amesema, mnada huo utashirikisha wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi na atakayenunua madini hayo katika mnada ni atakayeshinda bei iliyowekwa.

“Mnada huu utaendeshwa kwa usalama mkubwa kwa kuwa madini hayo hususan Tanzanite yana thamani kubwa. Serikali imeimarisha ulinzi ili kujihadhari na watu wasio waaminifu,”amesema Waziri Mavunde.

Aidha, amesema mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki na kodi kwa uwazi ili kuchangia pato la Taifa na kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji, wanunuzi na mali zao.

Minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya vito kama vile Zambia (emerald), Zimbabwe (almasi) na Afrika Kusini (almasi).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals